Habari kutoka nchini Ngeria zinasema kuwa mto maarufu kwa jina la Enugu uliopo kusini mashariki mwa nchi hiyo umevuta hisia za watu wa mataifa mbalimbali kwani inadaiwa kuwa mto huo unaponya wagonjwa kama vile ilivyokuwa nchini Tanzania kwa Babu wa Loliondo. Inasemekana kuwa watu kutoka mataifa mbalimbali wamefurika katika mto huo kupata tiba. Cha kushangaza zaidi ni kwamba mto huo una maji machafu na yananuka vibaya lakini wagonjwa wanazidi kumiminika ili kupata tiba kama unavyoona katika picha. Wapo tayari kupiga mbizi ndani ya maji hayo machafu tena yenye harufu mbaya kweli kweli.Ama kweli imani ni kila kitu.. TAZAMA VIDEO HAPA CHINI UONE HALI ILIVYO |
Social Plugin