MTOTO WA MIAKA MINNE ATUMBUKIA CHOONI NA KUFARIKI DUNIA HUKO TABORA
Thursday, February 27, 2014
Mwili
wa mtoto John Mwapwani (4)aliyefariki majira ya asubuhi baada ya
kutumbukia kwenye tundu la choo nyumbani kwao mtaa wa Sikanda kata ya Chemchem eneo la
Ally Hassan Mwinyi ndani ya Manispaa ya Tabora.
Inasemekana kuwa mtoto huyo mara baada ya kuamka asubuhi ,baba yake mzazi alimwambia
aende chooni kujisaidia kama ilivyo ada kwa wazazi wafanyavyo kwa
watoto wao,Mtoto John(4)alikwenda chooni.
Baada ya kimya cha muda mrefu kutawala baba wa mtoto huyo alielekea sehemu ya choo,lakini katika hali ya kusikitisha alikuta mwili wa mtoto huyo ukielea kwenye maji machafu
akiwa tayari amepoteza maisha.
Picha na kapipij blog
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin