Mwanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo cha Ualimu cha Winneba, nchini Ghana, amejiua kwa kujinyonga mara baada ya jina lake kubandikwa kwenye ubao wa matangazo (notice board) kuwa amefeli masomo matatu.
Jina la mwanafunzi huyo limehifadhiwa kwa sasa, ila inasemwa kuwa sababu ya kujinyoga kwake ni kutokana na kufeli masomo hayo matatu ambapo kungepelekea kufutwa kwake shule hapo.
Sababu hasa ya kifo chake haijajulikana moja kwa moja ila inaaminika ilitokana na hofu ya kutimuliwa chuoni hapo kutokana na kufeli mitihani mitatu.
Wilson Dabuo, ambaye ni muwakilishi wa wanafunzi kwenye baraza la chuo hicho, alieleza kupitia Joy News kwamba chuo hicho kina sheria ya kutimua wanafunzi wanaofeli masomo matatu kwenye mitihani yao.
Social Plugin