Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Huzuni kubwa!!MWANAMKE AUAWA BAADA YA KUKATAA KUTOA PENZI KWA MPENZI WAKE

Jeneza la Marehemu, Sekunda Mushi (42), aliyeuwawa kinyama usiku wa kuamkia, Januari 6, wakiwa na majonzi katika mazishi ya mwanamke huyo anayedaiwa kuuwa kwa sababu ya kimapenzi baada ya kuibuka kwa ugomvi kati yake na Mpenzi wake, aliyetajwa kwa jina la Gerald Mamkwe ambapo inadaiwa marehemu alikataa kutoa penzi kwa mpenzi wake huyo
Jeneza la mwili wa Marehemu Sekunda Mushi likiingizwa kaburini katika mazishi yaliyofanyika jana katika kijiji cha Longuo A, kata ya Uru Kusini, manispaa ya Moshi, mkoani Kilimanjaro.
Mzee Onesmo Mushi, ambaye ni Baba Mzazi wa Marehemu Sekunda Mushi, akiweka udongo katika kaburi la mwanamke huyo aliyeuwawa kinyama na mtu anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, kutokana na ugomvi wa kimapenzi
Mama Aurea Mushi, ambaye ni Mama Mzazi wa Marehemu Sekunda Mushi, akiweka udongo katika kaburi la mwanamke huyo aliyeuwawa kinyama na mtu anayedaiwa kuwa ni mpenzi wake, kutokana na ugomvi wa kimapenzi
Credit-
KIJIWE CHETU BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com