Mwanamke mmoja raia wa Uingereza amejifungulia katika
barabara moja mjini New York akiwa njiani kuelekea hospitali kutokana na
uchungu wa uzazi.
Polly McCourt, mwenye umri wa miaka 39,aliondoka
nyumbani kwake katika mtaa wa East Side siku ya Jumatatu na kujaribu
kukodisha taxi hadi alipogundua kuwa mwanawe asingeweza kusubiri.
Wapita njia walimpa mama huyo koti
na vitambaa walivyokuwa navyo kumfunika mwanawe hadi wahudumu walipofika
kumsaidia na kumpeleka hospitaliini.
Mama na mtoto walikuwa salama walipofikishwa hospitalini.
"alipiga mayowe akisema Mungu wangu mtoto wangu yuaja ,'' alisema shahidi mmoja.
Na niliweza kuona kichwa cha mtoto. Tulipomlaza mama chini kumsaidia, mtoto akawa tayari ametoka.''
Bi McCourt, anayetoka nchini Uingereza alijifungua mwanawe kando ya barabara.
Mama huyo alionekana akitabasamu alipoingia
katika gari la ambulensi na kupelekwa katika hospitali ya Lennox Hill
mjini New York.
Mumewe mama huyo alikuwa amekwama barabarani kutokana na msongamano wa magari alipopata simu kutoka kwa mkewe.
Wawili hao tayari wana watoto wengine wawili,
Conor mwenye umri wa miaka sita na Adele mwenye umri wa miaka minne
kulingana na jarida la New York Daily News.
Inaarifiwa walihamia mjini New York miaka minne iliyopita kutoka Dublin nchini Ireland.
>>via bbc swahili
>>via bbc swahili
Social Plugin