Ile Ziara ya wanamuziki Mad, Queen Durleen na Shilole imeingia doa kufuatia wananchi wengi kutokufurahishwa na uvaaji aliokuwa ameuvaa Shilole huku wazee wa Kisukuma na Kinyamwezi kumlani vikali mwanamuziki huyo na kudai siku akirudi tena huko aje amevaa gauni la sivyo atakiona cha moto.
Mtonyaji wetu wa habari hizi ambae alikuwa kwenye msafara wa wasanii hao aliieleza kuwa Shilole aliwafanya wakazi hao kushindwa kufurahia ujio wa wanamuziki hao kutokana na kinguo kifupi alichokuwa amevaa huku sehemu ya mapaja yake ikiwa wazi na watoto kushuhudia nusu mwili wake jambo ambalo hawajawahi kuona.
Hata hivyo Shilole ambae amekuwa na kawaida ya kuvaa nusu uchi akiwa stejini jambo ambalo mashabiki wengi wamekuwa wakichukizwa nalo na wamekuwa wakimuonya mara kwa mara kuachana na kuvaa nusu uchi kwa vile mashabiki wengi wanahitaji burudani na sio kuona maungo ya miili yake, lakini ameonekana kupuuza.
Xdeejayz ilimtafuta Shilole kupitia simu yake ya kiganjani ili azungumzie balaa hilo lililom kuta lakini kwa bahati mbaya hakuweza hadi habari hii inawafikia wasomaji wetu wenye kiu ya kujua habari na matukio yalijiri wikiend.
Social Plugin