Inadaiwa kuwa dada huyo alifika hospitali hapo akiwa yuko hoi hajitambui kufuatia kupata ajali ya pikipiki maarufu kama bodaboda hivyo kulazimika kukaa hospitali hapo karibia mwezi mzima..
Walioshuhudia tukio hilo walisema mtuhumiwa huyo alianza kukabidhi nguo zake kwa ndugu zake kila walipokuja kumuona .. na ndipo jioni alipooga na kuvaa kisista duu na kuondoka huku akiwaaga wagonjwa wengine kwamba anaenda kufanya mazoezi ya kutembea tembea.
Karibia masaa matatu yakapita bila dada huyo kurejea na ndipo dokta alipokuja kumdischarge na kukuta kitanda kitupu...
Akizungumzia tukio hilo mama mmoja ambaye anadai mara nyingi ana bahati ya kulazwa mara nyingi na dada huyo amedai ndiyo tabia yake na inabidi kusambaza picha zake kila hospitali hili asiendelee kutia hasara kwa kutapeli.
Social Plugin