Wakati mjadala wa Katiba Mpya hususani muundo wa Muungano
ukipamba moto, imebainika kuwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere
aliwahi kupendekeza kuanzishwa Serikali ya Tanganyika, kama sharti la
kuingia kwenye Shirikisho la Afrika Mashariki.
Maelezo hayo ya Mwalimu Nyerere yapo kwenye kitabu chake cha Uongozi
Wetu Na Hatima ya Tanzania kilichoandikwa mwaka 1994 na kutolewa 1995.
“Wakati Mwalimu anaandika kitabu hiki mwaka 1994 taifa letu lilikuwa
linakabiliwa na changamoto kadhaa za kihistoria ambazo ndizo zilimfanya
kuingilia kati na kuandika kijitabu hiki ambacho kilikuwa kama nasaha,
onyo, na usia kwa Watanzania,” inasema sehemu ya utangulizi wa kitabu
hicho.
Katika sura ya nne ya kitabu hicho, pamoja na mambo mengine Mwalimu
Nyerere alizungumzia suala la Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo
alieleza sababu zilizofanya muungano wa serikali mbili ukaanzishwa.
“Labda ni vizuri kukumbuka kwamba shabaha ya baadhi yetu ilikuwa ni
kuziunganisha nchi za Afrika Mashariki ziwe nchi moja,” alisema katika
kitabu chake hicho.
Alieleza kuwa, wakati Zanzibar na Tanganyika zinaungana, Kenya,
Uganda na Tanganyika zilikuwa katika mazungumzo ya kutafuta uwezekano wa
kuungana.
“Kama jambo hilo lingetokea, nina hakika kabisa kwamba mfumo wa nchi
mpya ambayo ingezaliwa ungekuwa ni wa shirikisho; ama shirikisho la nchi
tatu zenye serikali nne, au shirikisho la nchi nne zenye serikali tano.
“Kwa kweli hata kesho nchi za Afrika Mashariki zikiamua kuungana na
Tanzania ikawa ni mshiriki, naamini kuwa ni rahisi zaidi kushirikisha
Tanzania yenye serikali mbili ya Zanzibar na ya Tanganyika kuliko
Tanzania yenye serikali mbili, ya Tanzania na Zanzibar,” alisema.
Alisema kwa kufanya hivyo, wapendao Utanganyika watakuwa wazalendo
zaidi, badala ya kuwa wasaliti, wakiazimia Afrika ya Mashariki
iliyoungana kuwa nchi moja, kuliko Tanzania iliyotengana ikawa nchi
mbili.
Baadhi ya wahadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, wakizungumzia
suala hilo, walisema kuwa ni vyema kuangalia zaidi matakwa ya wananchi
kuliko kujali tu mfumo.
Mmoja wa wahadhiri hao, Faraja Christoms alisema wakati Mwalimu
Nyerere akiandika kitabu cha Uongozi Wetu Na Hatima ya Tanzania, alikuwa
na hofu ya kumeguka kwa muungano.
“Wakati ule kulikuwa na wale wabunge wa G55 jina walilobatizwa na
Profesa Issa Shivji, hawa wabunge walikuwa wanaona kama Zanzibar
inapendelewa sana, walikuwa wanaona kama wanalalamika tu kama watoto.
“Lakini ukiwasikiliza na wenyewe Wazanzibari walikuwa na hoja,
waliona kama Serikali ya Muungano ndiyo imekuwa ya Tanganyika kwa hiyo
vitu vya Muungano vilikuwa vinainufaisha zaidi Tanganyika,” alisema.
Alisema kutokana na hali hiyo ndiyo Mwalimu Nyerere alipoamua kuandika kitabu hicho.
Christoms alisema kwa mfumo wa sasa ulivyo ni vyema maoni ya Tume ya
Mabadiliko ya Katiba yakaheshimiwa, kwani hayatofautiani sana na yale ya
tume nyingine zilizowahi kuundwa kuangalia suala la Muungano.
Alisema kwa kuwa tayari Zanzibar ina katiba yake ambayo imetambua visiwa hivyo kama nchi, siyo rahisi kubadilisha hali hiyo.
“Ukisema tuendelee na serikali mbili, kero za Wazanzibari
hazitatatulika, ukitaka kulitatua hili kwanza useme haya mambo yasiyo ya
Muungano nani ayashughulikie na yale ya Tanganyika pia yatashughulikiwa
na nani?
“Mimi mwenyewe sioni kwa nini watu waseme tukiwa na serikali tatu
muungano utavunjika kwa sababu muungano ni ridhaa ya watu, kwa sababu
tayari Zanzibar ilishasema kuwa yenyewe ni nchi, Tume ya Warioba imebeba
mawazo ya watu kwa hiyo ni vyema tukayaheshimu,” alisema Christoms.
Kwa upande wake Dk Aldin Mutembi alisema, “Mimi sijaingia ndani sana
kwenye suala la serikali tatu ama mbili, lakini naungana na maoni ya
Tume ya Warioba.”
Tume ya Warioba ilipendekeza kuwapo kwa serikali tatu.
Mhadhiri wa Chuo cha Diplomasia, Dk Wetengere Kitojo alisema kuwa,
mawazo ya mwalimu yalikuwa serikali mbili kwa kuwa lengo lilikuwa katika
kuelekea kwenye muungano wa serikali moja.
Alisema kwa sasa baadhi ya watu wanapiga kelele kutaka uwepo wa
serikali mbili na wengine serikali tatu, ingawa ndani yake wapo ambao
hawautaki kabisa muungano.
“Serikali mbili ni muungano bora zaidi, tumekuwa na mfumo huu kwa
muda mrefu, lakini hatuoni kama kuna mwelekeo wa serikali moja, ndiyo
maana watu wengine wameona bora tuwe na serikali tatu ili tupunguze kero
ambazo zimeshindwa kutatuliwa kwa muda mrefu ndani ya mfumo wa serikali
mbili.
“Mimi naona cha msingi ni nia ya dhati, wapo wanaotaka serikali mbili
lakini hawana nia ya dhati ya muungano, wapo wengine serikali tatu
lakini pia hawautaki muungano.
Lengo ni muungano kamili, serikali tatu ni kurudi nyuma, ila sasa kama kwa miaka yote tumeshindwa kufikia lengo la serikali moja wengine wanaona bora turudi kwenye serikali tatu.
Lengo ni muungano kamili, serikali tatu ni kurudi nyuma, ila sasa kama kwa miaka yote tumeshindwa kufikia lengo la serikali moja wengine wanaona bora turudi kwenye serikali tatu.
Alisema kuwa, kwa mtazamo wake serikali mbili ni bora zaidi ili
baadaye iwepo moja lakini kama suala hilo limeshindikana ni bora kuwepo
na mfumo wa serikali tatu.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, Emanuel Muya alisema
mazingira yaliyomfanya Mwalimu Nyerere kuandika kitabu cha Uongozi Wetu
Na Hatima ya Tanzania, ni tofauti na haya yaliyopo leo.
“Pamoja na yote bado kuna umuhimu wa kuungana Tanganyika na Zanzibar,
hakuna anayetaka kuuvunja muungano, hata mwalimu alikuwa anataka
muungano imara, alivyoondoka muungano ulikuwa imara.
“Uwe unakubalika pande zote, kwa sa
sa una matatizo pande zote, lazima tukubali kupata mazingira aliyokuwa akiyataka Mwalimu,” alisema.
Via>>MWANANCHI
sa una matatizo pande zote, lazima tukubali kupata mazingira aliyokuwa akiyataka Mwalimu,” alisema.
Via>>MWANANCHI
Social Plugin