NB-picha haiendani na tukio |
Mkulima mwenye umri wa miaka 45 amefariki dunia baada ya kubugia kiasi kikubwa cha pombe haramu kwenye shindano la unywaji pombe, katika kijiji cha Kiegucu, wilayani Embu Kaskazini nchini Kenya.
Bw Mugo wa Karinga alikuwa amebishana na mwenzake kwamba angelipa bili yake ya chupa nne za pombe hiyo kali ikiwa angezinywa kavu bila kuchaganya na soda.
Pia alikuwa apokee Sh 200 ikiwa angemaliza chupa hizo zote.
Lakini alipomaliza chupa ya tatu, mwanamume huyo alizirai na kupata shida kupumua.
Mmoja wa watu aliyeshuhudia alisema badala ya kumsaidia walevi wengine walianza kushangilia wakidhania anajifanya tu.
“Walimzingira na kumhimiza amalize chupa ya nne. Pombe hiyo ni kali sana huwezi kuinywa bila soda ama maji,” alisema Bw Martin Mukundi.
Lakini baada ya dakika chache waligundua kwamba amezirai na ndio wakampeleka kwa zahanati ya Kianjokoma ambapo aliaga dunia. Mwili wake ulipelekwa kuhifadhiwa katika mochari ya hospitali kuu ya Embu
Social Plugin