Akisoma uamuzi wa kuwaachia watuhumiwa
hao wanaokabiliwa na kesi ya kuwashambulia kwa mapanga wafuasi sita wa CCM
hakimu mkazi mfawidhi wa wilaya ya kahama Gadiel Mariki amesema kwa makosa kama
hayo dhamana yake huwa iko wazi.
Mariki amesema kuzuia dhamana inategemea
na mwenendo wa
mashtaka ambapo katika cheti cha kiapo cha kuzuia
dhamana hiyo kilichotolewa na polisi masuala ya msingi hayakuzingatiwa na
kufanya hati kuwa batili.
Amesema kufuatia mapungufu hayo ikiwa ni
pamoja na maelezo ya wagonjwa watatu kuwa mahututi haijaonesha mtoaji wa
taarifa hiyo ninani hivyo hati hiyo ni batili.
Pamoja na kubatilisha hati hiyo na
kuweka dhamana wazi, wadhamini wa watuhumiwa 12 akiwamo diwani wa kata ya
Buselesele wamekosa sifa na kufanya warudishwe gerezani, huku wadhamini wa
mbunge kasulumbayi hati zao zikiwa sawa.
Kasulumbayi na wenzake wanashitakiwa kwa
makosa sita yakiwamo matano ya kujeruhi na moja la kuharibu mali za wanachama
wa CCM katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani kata ya ubagwe, na kesi hiyo
itatajwa tena feburuali 20 mwaka huu.
Social Plugin