Baadhi ya watumishi katika halmashauri ya manispaa ya
Shinyanga wamedaiwa kuihujumu kwa kutumia
mbinu ya kufungua kesi dhidi ya manispaa hiyo na kuiba nyaraka za ofisi ili
kujipatia kipato kinyume cha taratibu na maadili ya kazi.
Akizungumza katika
kikao cha baraza la madiwani wa manispaa hiyo,kilichofanyika jana katika ukumbi
wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga, mwenyekiti wa baraza hilo ambaye pia
naibu mstahiki meya wa manispaa hiyo David Nkulila(PICHANI HAPO JUU) alisema
halmashauri hiyo tofauti na siku za nyuma sasa inaandamwa na kesi nyingi za
ajabu ajabu zenye lengo la kuihujumu.
“Manispaa ya Shinyanga hivi sasa inataka kuchezewa na baadhi ya watu kwa
kuanzisha makosa yasiyoeleka dhidi ya manispaa na mujibu wa taarifa
zinazohisiwa,zinazotia mashaka hujuma hizo zinafanywa na watumishi wa
halmashauri”,alieleza mwenyekiti wa baraza hilo bwana Nkulila.
“Data zinazohisiwa,zinazosemekana,zinazotia
mashaka,watumishi wanahusika,Kesi nyingi sasa zinataka kuiandama
halmashauri,mdau yupo anaambiwa anzisha kesi na kesi inaenda kushindikana,mtu
huyo anadai alipwe na halmashauri, na hayo madai yanavyosemekana ni mgao wa
watu,hizo ni hujuma kwa pesa za wananchi”,alisema Nkulila.
Akifafanua zaidi alisema menejimenti ya manispaa hiyo imekosa
nidhamu ya siri kwani wamekuwa wakitoa nyaraka za siri na kwamba sasa wamebuni
njia nyingine ya ulaji kwa kuanzisha kesi badala ya kuwajibika.
“Katika uongozi wangu haya nimeyaona,hata mkurugenzi wa
halmashauri wa manispaa ni shahidi,mtu anacheza na kitu anachojua kabisa kuwa
ni makosa,anaiba nyaraka ,akishaiba anaenda wanashauriana na wenzake ,analeta
malalamiko,akitaka nini alipwe ”,alieleza Nkulila.
“Zimeanza kuibuka kesi ambazo katika halmashauri
haziwahi kutokea,hizi ni hujuma tu,hujuma ya nini?,ulaji!,ulaji kivipi? nyofoa
nyaraka hii....,hili lazima tulikemee,lazima tuliseme,tutakwenda nao sambamba,mimi
niko pale nimepewa dhamana ninayaona kila siku,hawa hawhitaji kuletwa kwenye
baraza ni kuwapeleka mahakamani tu”,aliongeza naibu meya huyo.
Aidha alisema aina hiyo ya wizi inatokana na pale
watendaji wanapowajibishwa na inapotokea kibano cha ulaji katika kila eneo
kimeshindikana, basi wameamua kubuni njia nyingine ya ulaji kwa kufungua kesi
za ajabu ajabu dhidi ya manispaa ili mwisho wa siku walipwe mamilioni ya fedha
ambayo kimsingi ni mali ya wananchi.
Akizungumza katika kikao hicho katibu tawala wa wilaya
ya Shinyanga Boniface Chambi alieeleza kukerwa na tabia hiyo na kuwataka
watumishi wa umma kutunza siri za ofisi na endapo mtu anaona kazi ya serikali
ni ngumu basi aache badala ya kuchezea nyaraka za serikali.
Social Plugin