Wanawake wawili wameuawa na waume zao katika matukio mawili yaliyohusisha mmoja kukatwa koo na mumewe.
Wanandoa hao waliuawa wilayani Chunya mkoani Mbeya, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya Ahmed Msangi.
Kamanda alieleza kuwa Agnes Daudi, anadaiwa kuuawa na mumewe Thomas Msukuma na kwamba mwili wake ulikutwa ukiwa umekatwa koo na kutelekezwa kwenye kibanda walichokuwa wakiishi pamoja enzi za uhai wake.
Alisema tukio hilo lilitokea saa 1:00 asubuhi katika kijiji cha Shoga wilayani Chunya.
Katika tukio la pili lilitokea saa 12:00 jioni kijiji cha Landan Dafroza Gidion (18) aliuawa kwa kupigwa ngumi na mateke mashambulio yaliyodaiwa kufanywa na mumewe Juma Januari.
Alisema sababu za mauaji hayo ni chuki za mapenzi.
CHANZO: NIPASHE
Social Plugin