Dada
mmoja anayedaiwa kuwa mkazi wa jijini Dar es Salaam ameuawa kinyama
baada ya kubakwa hadi kufa eneo la Nanenane ndani ya mashamba ya mikonge
mjini Morogoro.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema kuwa, mrembo huyo ambaye hakufahamika aliuawa kwa kubakwa na watu wasiojulikana ambapo maiti yake ilikutwa ikiwa imevuliwa nguo za ndani.
Aidha, kwenye shingo yake kulikutwa na kitambaa ambacho inadhaniwa kuwa ndicho kilichotumika na wahalifu kumnyongea.
Baada ya polisi kukagua pochi
yake walikuta ikiwa na tiketi iliyoonyesha kuwa alisafiri kutoka Dar es
Salaam hadi mjini hapa bila kuwa na jina la msafiri.
Baadhi
ya wananchi walioshuhudia maiti hiyo, wamesikitishwa na tukio hilo.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, ACP Faustene Shilogile
alipohojiwa juzi na mwandishi wetu alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Nawaomba watu wanaomfahamu marehemu huyu wafike chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mkoa wa Morogoro kumtambua,” alisema Shilogile.
credit-kandili yetu leo
Social Plugin