Ukatili dhidi ya wanawake umeendelea kufanyika katika jamii ambapo huko mkoani
Simiyu mwanamke mmoja aitwaye Minza Noni (56) ameuawa kikatili kwa kukatwa mapanga titi lake la kushoto na watu wasiojulikana kisha kutokomea nalo
kusikojulikana.
Tukio hilo limetokea usiku wa
kuamkia siku ya Jumamosi wiki iliyopita majira ya saa sita usiku katika
kitongiji cha Nyasiri kijiji cha Isiyu kata ya Girya wilayani
Bariadi mkoani Simiyu.
Mkuu wa upelelezi mkoa wa Simiyu ACP Evance Mwijage amesema mwanamke
huyo akiwa nyumbani kwake alivamiwa na kukatwa
mapanga na watu hao kisha kumkata panga kwenye titi lake la kushoto na kutoweka
nalo kusikojulikana na kwamba jeshi hilo
la polisi linaendelea kufanya uchunguzi
zaidi juu ya tukio hilo.
Social Plugin