Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la
Pendo Ladislaus (28)mkazi wa mtaa wa Lwenge wilayani Geita (PICHANI)amemwagiwa mafuta ya
moto na kuunguzwa vibaya sehemu za kifuani na tumboni baada kuhitirafiana na
mama mwenye nyumba alipopanga aitwaye Bi Leticia Charles.
Tukio hilo limetokea Januari 31 mwaka huu
majira ya saa kumi jioni.
Mganga mfawidhi wa hospitali ya wilaya ya
Geita Dk Adam Sijaona amethibitisha kumpokea mama huyo na amelazwa wodi namba
saba na hali yake inaendelea vizuri.
Na Valence Robert-Geita
Social Plugin