Chama cha mapinduzi CCM kimeibuka mshindi katika uchaguzi mdogo wa udiwani katika kata ya Ubagwe wilayani Kahama ambako siku chache kabla ya Uchaguzi WANACCM 6 walicharangwa mapanga na watu wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa Chadema. Vyama vitatu vya siasa vilikuwa vimesimamisha wagombea. Matokeo ya uchaguzi uliofanyika jana ni kama ifuatavyo- 1.Hamis Majohoro wa CCM kura 323 2.Adam Ngoma wa CHADEMA kura 219 3.Majija Lubinza wa TADEA kura 95 Msimamizi wa uchaguzi huo alikuwa Sospeter Alseco |
Social Plugin