Yule kijana aliyemuua mama yake kwa kumkata jembe kichwani juzi na
kusababisha kifo chake papo hapo huko katika kijiji cha Mwakuhenga wilayani
Kahama mkoani Shinyanga anashikiliwa na jeshi la polisi.
Kaimu kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, mrakibu mwandamizi wa Polisi,
Juma amemtaja mwanamke aliyeuawa kuwa ni Munde Luchagula (48-50) ambaye
alikatwa jembe na mwanaye Mbogo Charles (34) wakati akiandaa chakula cha usiku.
Amesema chanzo cha mauaji hayo bado hakijafahamika japokuwa inahisiwa
mtuhumiwa alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa akili na tayari anashikiliwa na
jeshi la polisi na atapimwa ili kubaini ukweli
Social Plugin