Mkuu
wa Wilaya ya Mjini Unguja Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Kiongozi
wa Kanisa la Mkunazini Ndg. Nuhu Salanya, na Maofsa wa JWTZ , katika
eneo la tukio na kutoa maelekezo kwa Uongozi wa Kanisa walipofika katika
eneo la tukio kuangalia athari na uharibifu uliotokea katika eneo hilo,
wakati wa mripuko huo.
Mkuu
wa Wilaya ya Mjini Mhe Abdi Mahmoud Mzee akizungumza na Makamanda wa
JWTZ waliofika eneo la tukio kuangalia na kuchunguza tukio hilo la
mripuko katika eneo la Mkunazini jirani la Kanisani.Maofisa wa JWTZ wakiangalia eneo la tukio lililochimbika kutokana na kitu kinachodhaniwa ni bomu
Polisi Visiwani Zanzibar wamethibitisha kutokea milipuko mitatu ya mabomu kati ya Jumapili na Jumatatu leo mchana visiwani humo.
Mkuu wa Polisi Zanzibar, Hamdan Omar Makame amesema milipuko
miwili imetokea leo katika eneo la mgahawa wa Mercury huku mlipuko
mwingine ukiwa umetokea katika eneo la Mkunazini, ikifuatia mlipuko
uliotokea siku ya Jumapili wiki iliyopita katika eneo la Pangawe.
Mkuu huyo wa Polisi Zanzibar amesema kuwa hakuna
vifo wala majeruhi katika matukio yote matatu wala mali iliyoharibiwa,
isipokuwa madhara ya kisaikolojia kutokana na hofu na taharuki kutokana
na matukio hayo.
Aidha mkuu huyo wa Polisi ameeleza kuwa upelezi unaendelea ili kuwabaini waliohusika katika matukio hayo ingawa hadi wakati huu hakuna mtu au mshukiwa yeyote aliyekwishamatwa kuhusiana na matukio hayo.
Kuhusu hatua za tahadhari kufuatia matukio hayo Kamanda Makame amesema Polisi wanaendelea kuimarisha ulinzi katika sehemu mbali mbali visiwani humo ikiwa ni pamoja na kufanya doria katika maeneo kadhaa na amewaondoa hofu wananchi wa visiwa hivyo kuhusu usalama wao.
Social Plugin