Sakata la wanafunzi wa shule ya Sekondari
Nyugwa katika kata Nyugwa wilayani Nyangh’wale mkoani Geita kuhusu kupewa
majina ya bandia limechukua sura mpya baada ya wanafunzi hao kukubalina kufanya
maandamano makubwa kwenda kwa mkuu wa mkoa wa Geita Saidi
Magalula endapo serikali haitawachukulia hatua mwalimu mkuu wa shule
hiyo pamoja na afisa elimu wa sekondari kwa kuuza majina ya wenzao 11 na kuwapa
majina bandia.
Hatua hiyo ya kufanya maandamano
imeafikiwa leo baada ya afisa elimu wa sekondari wa wilaya Bi, Mosha kufanya
kikao katika ukumbi wa shule hiyo na kuwaambia wanafunzi wote 11
walifutiwa matokeo yao kwa kukosa majina yao hawatakiwi kuonekana
shuleni kwani wakiendelea kukaa hawatafanya mtihani wa kidato cha nne na wazazi
wao wanatakiwa watafute utaratibu mwingine.
Kitendo cha afisa elimu huyo kufanya kikao
na kuwaambia wanafunzi
11 hawatakiwi kuonekana katika maeneo ya shule kimezua taaruki kubwa kwa
wanafunzi pamoja na wazazi waliokuwemo kwenye kikao hicho huku ikidaiwa kuwa yeye mwenyewe ndiye
aliyewaamuru wafanye mtihani kwa kutumia majina yasiyo yao katika mtihani wa
kuingia kidato cha tatu mwaka jana na kuahidi kuwasaidia na
mpaka sasa hajachukua hatua hivyo kuonekana
yeye anahusika na mkuu wa shule hiyo kuuza majina ya watoto wao na kuwapa ya
bandia tena kwa pesa kuanzia shilingi(25000) hadi (30000) na kudai majina yao
ya awali yako mkoani yanatakiwa yatafutwe.
Mmoja wa wanafunzi aliyebadilishiwa jina
lake la awali alikuwa anaitwa Jen Pendo na kubatizwa la badia la Jasinta Zakaria
alikuwa na haya ya kusema..........
“Nashangaa
kuona afisa elimu anatugeuka na huku yeye ndiye aliyetusaidia kufanye mtihani
na aliahidi kuwa atalishugulikia na an hawatutakiwi kuonekana
katika shule hii bali wazazi wafanye utaratibu mwingine.’’
“Kwa kweli namshaanga huyu afisa elimu
kwani mimi mwenyewe nilikataa baada ya kuona jina si langu lakini akaniomba
nilifanyie jina hilo na atalishugulikia nashangaa hata mimi ananigeuka ,sasa niende
wapi na nimepoteza muda mwingi na kulipa michango yote na je pesa yangu
watarudisha? naiomba serikali ituasaidie kutatua mgogoro huu ‘’alieleza Jen
Pendo
Wakati huohuo wazazi waliokuwepo
kwenye kikao hicho cha wanafunzi na walimu wa shule hiyo
wamlalamikia kitendo hicho na kukiita cha kinyama na cha kikatili huku nao
wakiomba serikali kuingilia mgogoro huo na kuwachukulia hatua kali na
ikiwezekana wapewe adhabu kali ama wafukuzwe.
“Mimi kama mzazi naona mwalimu hawezi kuuza majina peke
yake ,maafisa elimu wote naona watakuwa wanajua wote wachukuliwe hatua lakini pia
nashanga kuona mwalimu mkuu bado yupo hapa na wakati amefanya hujuma zote hizi”,alisema
mzazi aitwaye Pendo kisabo.
Social Plugin