Maandamano ya kupinga agizo la wanawake kutovalia sketi fupi nchini Uganda
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia saini sheria mpya inayotoa adhabu
kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutembea nusu uchi au kuhusika na vitendo
vinavyohusisha picha zenye watu uchi.
Wanawake pia wamezuiwa kabisa kuvalia sketi fupi sana au 'Mini Skirt' kama
zinavyojulikana au blausi ambazo zinaonyesha kifua chao hadharani na
kusababisha hisia za kingono .
Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama hizo zitakubalika tu ikiwa zinatumika
kwa ajili ya mafunzo au wakati wa michezo na hafla za kitamaduni.
Akihutubia waandishi wa habari, mjini Kampala, waziri wa maadili na utawala
bora, Reverend Simon Lokodo alisema kuwa Rais Museveni alipitisha sheria hiyo
tarehe 6 mwezi huu, miezi mwili baada ya bunge kuipitisha.
Kwa mujibu wa sheria hiyo kamati dhidi ya vitendo hivyo itabuniwa ili iweze
kutekeleza sheria hiyo kwa kuhakikisha kuwa picha, au video zenye watu uchi
zinanaswa na kuharibiwa.
Kamati hiyo, itajumuisha watu kutoka katika sekta mbali mbali ikiwemo ya
habari na utumbuizaji.
Sheria hiyo inasema kuwa mtu yeyote atakayepatikana akijihusisha na vitendo
cya watu kuwa uchi, kuvalia nusu uchi , kuona sinema za watu wakiwa uchi au
kuchapisha picha za watu walio uchi kwa lengo la kuleta hisia tofauti
utachukuliwa hatua kali za kisheria.
Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu kuvalia nguo zisizo na heshima na
kuzua hisia zisizofaa miongoni mwa watu.
Watakaopatikana wakivunja sheria na kuvalia visivyo watafungwa hadi miak 10
na wale watakaopatiokana na hatia ya kuhusisha watoto katika biashara ya ngono
watafungwa hadi miaka 15.
Chanzo-BBC Swahili
|
Social Plugin