Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAFANYAKAZI SHINYANGA KUFANYA MAAJABU SHEREHE ZA MEI MOSI 2014,FUATILIA HAPA KIKAO CHA WADAU WA MEI MOSI KILICHOFANYIKA LEO MJINI SHINYANGA KUCHANGIA SHEREHE HIZO KIMKOA

Katikati ni mwenyekiti wa Shirikisho  la vyama vya wafanyakazi TUCTA mkoa wa Shinyanga bwana Fue Mrindoko akizungumza leo katik kikao cha wadau wa sherehe za  Mei Mosi mwaka 2014 mkutano uliofanyikia katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa Shinyanga ikiwa ni katika mikakati ya wafanyakazi mkoa wa Shinyanga kuchangia sherehe za Mei Mosi.Mrindoko alisema katika mikakati ya kufanikisha sherehe hizo ambazo katika mkoa wa Shinyanga mwaka huu zitafanyika katika wilaya ya Shinyanga baada ya Kahama mwaka jana wamejipanga kikamilifu ili sherehe hizo ziwe za mfano wa kuigwa hapa nchini
Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akizungumza katika kikao hicho ambacho kimehudhuriwa na wadau wengi wa Mei mosi,ambapo pamoja na mambo mengine alizitaka mamlaka zinazohusika na uaandaaji wa zawadi kwa wafanyakazi bora zifanye kazi ya kuteua wafanyakazi bora kwa kuzingatia vigezo vinavyotakiwa lakini pia bila kuingiliwa na mtu yeyote.Mkuu huyo wa mkoa alisema hatarajii ofisi yoyote kukosa mfanyakazi bora lakini pia akisisitiza vyombo vya habari kuwa ni wadau muhimu katika kufanikisha sherehe hizo muhimu kwa wafanyakazi

Katikati Mkuu wa mkoa akizungumza katika kikao hicho.Wa kwanza kulia ni kaimu katibu tawala msaidizi na rasiliamali watu wa mkoa wa Shinyanga bwana Kajia Godfey,wa pili ni katibu tawala mkoa bi Eva Loppa.Wa kwanza kushoto ni mratibu wa TUCTA mkoa wa Shinyanga,ambaye pia ni katibu wa chama cha wafanyakazi serikali kuu bi Tabu Mambo,akifuatiwa na mwenyekiti wa TUCTA mkoa wa Shinyanga Fue Mrindoko

Kikao kinaendelea,wa kwanza ni kulia ni mkuu wa wilaya ya Kishapu Wilson Nhambaku ,akifurahia kitu ndani ya kikao hicho,wa pili ni mkuu wa wilaya ya Kahama Benson aliyekuwa mwenyeji wa sherehe za Mei Mosi mwaka jana 
Aidha kabla ya kilele cha sherehe hizo za mei mosi kutakufanyika michezo  mbalimbali kama vile mpira wa miguu,mpira wa pete,bao na karata,kuvuta kamba,kukimbiza kuku,riadha na mbio za baiskeli na michezo kadha wa kadha siku ya kilele cha sherehe hizo

 Mratibu wa TUCTA mkoa wa Shinyanga,ambaye pia ni katibu wa chama cha wafanyakazi serikali kuu bi Tabu Mambo akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema miongoni mwa wadau wa sherehe hizo ni viongozi wa vyama vya wafanyakazi,wafanyakazi,waajiri pamoja serikali na siku ya sherehe za mei mosi zawadi mbalimbali zitatolewa kwa wafanyakazi bora katika sekta binafsi na zawadi itaanzia shilingi 300,000/= na kuendelea,sekta za umma zawadi itaanzia shilingi 500,000/= na kuendelea,sekta ya migodi ya kati shilingi 500,000/= na kuendelea na sekta ya migodi ya mikubwa zawadi itaanzia shilingi 1,000,000/= na kuendelea
Awali akisoma taarifa ya wadau wa sherehe za Mei Mosi mwaka huu katika mkoa wa Shinyanga,katibu wa TUICO mkoa wa Shinyanga bwana Fabian Samkumbi (hayupo pichani) alisema wadau wa kuchangia sherehe hizo ni Vyama vya wafanyakazi kama vile TUGHE mkoa,CWT,TAWLGU,TPAW,TAMICO,CHODAWU,TUICO,CWT wilaya/Manispaa Shinyanga,CWT Kishapuna Kahama,RAAWU,TRAWU,TEWUTA,TTCL,COTWU.Wadau wengine aliwataja kuwa ni waajiri taasisi za serikali-TUGHE,wakurugenzi wa halmashauri za wilaya CWT,TUGHE na TALGU,wajiri wa sekta binafsi CWT,waajiri kutoka TAMICO,wajiri kutoka RAAWU,CHODAWU,TUICO,TPAWU,COWTU(T),TEWUTA na waajiri kutoka TRAWU
Kikao kinaendelea
Wajumbe wa kikao wakisikiliza kilichokuwa kinaendelea ndani ya ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Ukumbi huo wa mikutano ulikuwa umejaa sana tofauti na vikao vingine ambavyo hufanyika katika ukumbi huo
Ni katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga wajumbe wa kikao hicho wakifuatilia mawili matatu yaliyokuwa yanajiri katika kuhakikisha kuwa sherehe za mei mosi zinakuwa za mfano hapa nchini mwaka huu

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com