Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MWANAMME AUAWA BAADA YA KUMUUA BABA YAKE MZAZI

NewsImages/2213346.jpg
Mwanamme mmoja ameuawa na wanakijiji muda mchache tu baada ya kumuua babake kwenye kisa ambacho kiliwashangaza wakazi wa kaunti ya Nyamira nchini Kenya.

Mshukiwa huyo, Bw Nyairo Nyaenya, 26 alimchoma kisu babake Bw Joseck Nyaenya Orobi, 60 naibu wa kamati ya kudumisha usalama vijijini (Community Policing) katika kijiji cha Omwaro na kumuua papo hapo.

Mshukiwa huyo baadaye alijifungia ndani ya nyumba yake na mwanawe wa kiume wa miaka kumi na kutisha kumuua kama yeyote angemfuata huko na kujaribu kumdhuru.

Lakini mama wa mshukiwa huyo Bi Yusavia Nyaenya alipiga nduru na wanakijiji waliofika hapo walivunja na kuingia ndani ya nyumba na kumuua mshukiwa huyo na kumuokoa mtoto aliyekuwa ametekwa nyara.

Kitu cha kushangaza ni kuwa wanakijiji hao walitaka kumuua pia mtoto huyo waliyemuokoa wakisema hawakuwa wanataka kizazi cha mshukiwa huyo kiendelee kwa sababu ya vituko vingi alivyokuwa ametenda katika kijiji hicho.

Lakini kwa bahati nzuri kamanda mkuu wa kituo cha polisi cha Nyamira Bw David Muange na naibu wa chifu wa kata ndogo ya Bigege Bw Justus Okenye waliokuwa wamefika mahali hapo walimwokoa mtoto huyo.

Damu ya mbwa
Kabla ya Bw Nyairo kumuua babake, alichinja mbwa na kunywa damu yake, kisa ambacho kiliwashangaza babake na mamake.

Pia alikatakata migomba kwenye shamba la familia hiyo.
Bw Okenye alisema taharuki ilitanda wakati Bw Orobi alijaribu kujua ni kwa nini Bw Nyairo alikuwa na tabia isiyoleweka.

 “Nyairo ambaye alikuwa amejihami kwa panga na kisu alianza kumkimbiza babake. Kwa bahati mbaya mzee huyo alianguka na kuawa hapo hapo,” Bw Okenye alisema.
Alisema hivi karibuni, Bw Nyairo alikuwa ameua ng’ombe wao bila sababu yoyote.

“Mkewe mshukiwa huyo aliachana naye kwa sababu ya tabia yake isiyoeleweka,” Bw Oknye alisema.
Kis hicho kilitendeka katika kata ya Bosamaro Chache kwenye eneobunge la Mugirango Magharibi kiliwashangaza wakazi wa eneo hilo.


Miili wa wawili hao ilipelekwa katika mochari ya hospitali kuu ya Nyamira nchini Kenya.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com