Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WATATU WAHUKUMIWA KIFO BAADA YA KUMBAKA KWA ZAMU MSICHANA,YADAIWA ALIWATOSA WAKAAMUA KULIPA KISASI

Eneo ambapo msichana huyo alibakwa kwa siku tatu kabla ya kuuawa
Wanaume watatu wamehukumiwa adhabu ya kifo nchini India baada ya kupatikana na hatia ya kumbaka 'mande' msichana mwenye umri wa miaka 19. 

Mahakama mjini Delhi ilielezwa msichana huyo alitekwa nyara na wanaume hao watatu katika eneo la Qutub Vihar mjini humo wakati akirejea nyumbani kutoka kazini mjini Gurgaon.

Mwili wake ulioharibika vibaya uligundulika siku tatu baadaye mjini Rewari, Haryana, imeripotiwa.
Mahakama ilielezwa msichana huyo alipigwa na kumwagiwa tindikali kwenye macho yake.

Upande wa mashitaka ulisema wanaume hao, wawili kati yao wakiwa ndugu, walimbaka kwa zamu na kumshambulia binti huyo kwa zaidi ya siku tatu hadi alipofariki mnamo Februari 2012, imeripotiwa.

Mahakama ilielezwa wanaume hao walipanga kulipa kisasi baada ya msichana huyo kukataa alipotongozwa na mmoja wa vijana hao.
Wiki iliyopita mahakama ilimtia hatiani Ravi, Rahul na Vinod katika moja ya kesi chache zinazotokea kwa nadra mno.
Zaidi ya watu 100, wakiwamo ndugu wa msichana huyo na majirani, walikusanyika nje ya mahakama hiyo kila mara inaposikilizwa kesi hiyo kutaka adhabu kali dhidi ya watuhumiwa hao.

Polisi wa mini Delhi wameshinikiza adhabu ya kifo kwa wanaume hao, ambao walitiwa hatiani Ijumaa. Mahakama hiyo ilielezwa hakuna peyote kati ya watuhumiwa hao aliyeonesha kujutia wakati wa kusomwa hukumu hiyo.

Mama wa msichana huyo mapema wiki hii alieleza hakuwa na huruma moyoni mwake kwa wanaume hao watatu ambao walimbaka kinyama na kumuua binti yake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com