Sakata la wizi wa mabati 14 ya jimbo
yaliyotolewa na mbunge ,linalomkabili diwani wa kata ya Chigunga Hoja
Mlyakado limechukua sura mpya baada ya mwenyekiti wa chama hicho mkoani Geita
Joseph Msukuma kumtaka awajibishwe mara moja kwa kitendo alichokifanya
kwani ni fedheha mbele ya chama na mbele ya jamii nzima.
‘’Mimi kama mwenyekiti wa chama sijawahi
kuona kiongozi ambaye ni mwakilishi wa wananchi na mwizi kama huyo inatakiwa
awajibishwe mara moja na mimi nitahakikisha anawajibishwa kwa mujibu wa katiba
ya chama cha mapinduzi”,alisema Msukuma.
“Kuanzia sasa hivi nitaagiza mamlaka
zilizo chini yangu kuweza kulishughulikia suala hili kwa sababu nilikuwa
silijui kama kuna kitu cha namna hii nashukru kunipa taarifa hizi ili hatua
ziendelee kuchukuliwa”,aliongeza Msukuma.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa ccm mkoa wa Geita amesema chama
cha mapinduzi hakikubaliani na viongozi wezi na wasiokuwa na maadili ndani ya
chama na yeyote akibainika atachukuliwa hatua kali na ameahidi kuwagiza viongozi wa ngazi ya
wilaya wachukue hatua kali dhidi ya diwani huyo mwizi haraka iwezekanavyo.
Ni hivi karibuni wakazi wa mji wa Geita na
vitongoji vyake walishangazwa na kitendo cha Diwani wa kata ya Chigunga kuiba
mabati 14 yaliyotolewa na mbunge wa jimbo hilo Mh Lolesia Bukwimba na
baadaye mbunge huyo kumwagiza diwani huyo ayarudishe mabati
hayo baada ya kukiri katika mkutano wa hadhara kuwa aliyachukua.
Wakiongea kwa nyakati tofauti na mwandishi
wa habari hizi wananchi wa mkoa na vitongoji vyake wamesema kitendo cha diwani
huyo kuiba mabati 14 na kufanya mkutano na kuwaambia wanananchi kwamba ameleta mabati 86 na 14 yatakuja na
mbunge si cha kiungwana na kitendo cha kuwafedhehesha wengine wanaoleta
maendeleo kwenye kata zao huku baadhi ya viongozi wakiwa wanaiba.
Kwa upande wa viongozi wa vyama
vya upinzani akiwemo kaimu katibu wa CHADEMA mkoani Geita Logers Luhega
amesema kitendo cha diwani huyo kuiba mabati kumi na nne na kumsingizia mbunge
wake si chakiungwana na kuwaomba viongozi wa CCM mkoa wa Geita kumchukuli
hatua kali diwani huyo kwa wizi huo kwani amekidharirisha chama na
wananchi wamekosa imani naye.
‘’Kama diwani anafanya wizi kwa kuwaibia
wananchi wake, je wengine wafanyeje? na kama hawatachukua hatua kali kwa diwani
huyo tutahisi na wao wanahusika kuona mali za wananchi zinaibiwa”,alisema
katibu huyo wa CHADEMA’.
Sakata la kuwepo kwa tuhuma za wizi wa
mabati 14 zilianza kutolewa kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kayenze
baada ya wananchi kumhoji mbunge kuwa mabati 14 je amekujanayo? kama ambavyo
diwani huyo aliwaahidi wananchi kuwa alileta mabati 86 na mengine mbunge
atakuja nayo.
Kufuatia maswali ya wananchi,kitendo hicho
kilimshitua mbunge huyo na kusema.....
“Mimi
nilitoa mabati 100 tena ya geji 28 nashangaa kuniambia nimekuja na mabati14
ndipo alipomsimamisha diwani huyo na kuanza kuzomewa na wananchi kwa kitendo
alichokifanya cha kunisingizia kumbe yeye ameyachukua”,alisema mbunge huyo.
Na Valence Robert-Geita
Social Plugin