|
Jana mchana kikosi cha waandishi wa habari kilifanya ziara ya ghafla kutembelea maeneo mbalimbali katika manispaa ya Shinyanga na kujionea hali halisi ya mazingira mengi yakiwa yameghubikwa na uchafu wa hapa na pale,huku wananchi wakiwa hatarini kupatwa na magonjwa ya aina mbalimbali,lakini wengine wakihofia pengine kunaweza kutokea mafuriko kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha kwani hali ya miundombinu hairidhishi,TAZAMA PICHA ujioneee mwenyewe mwanzo hadi mwisho wa ziara hiyo fupi.Tulianzia katika eneo la barabara inayotokea Bakurutu hadi eneo la TRA,Uhuru Sekondari.Picha hapo juu ni mtaro wa kupitishia maji unaotoka eneo la SHY-COM cha kushangaza mtaro huo umeishia eneo la Shule ya Sekondari Uhuru kama unavyoona hapo pichani.Pengine jiulize Je maji yanayotoka eneo la Shycom,Mnara wa voda,Bakururu baada ya kufika eneo hilo yanakwenda wapi !kwani hakuna mtaro mwingine unaoungana na mtaro huo kuchukua maji hayo! Tafadhali Fuatilia ziara hii ya wana habari katika mkoa ambao una kila aina ya utajiri na sasa viwanda vya kila aina vinaendelea kujengwa..... |
|
Katikati ya mji/mjini Shinyanga eneo la benki ya posta maji yakiwa yametuama baada ya mvua kunyesha hapo jana |
|
Eneo la mtaa wa Sukari mjini Shinyanga |
|
Hapa ni katika eneo la Nguzo nane mjini Shinyanga,mkabala kabisa na soko la Nguzo nane,eneo hili limezungukwa na MADUKA YA NYAMA(Bucha) kama unavyoona hapo pichani uchafu upo kwenye ndoo,beseni na boksi wakati huo huo duka la nyama likiwa karibu kabisa na duka la nyama na biashara inaendelea.Je usalama wa afya ya watumiaji wa nyama hiyo upo?, na wahusika wa mambo ya afya wameridhika na hali hiyo?,endelea kutafakari ...... |
|
Biashara inaendelea nje ya soko la Nguzo nane,maji machafu yakitoka ndani ya soko,cha kushangaza ambacho kila mtu kilimwacha mdomo wazi ni kwamba maji hayo mbali na kutoka katika soko hilo,PIA yanatoka katika CHOO kilichopo sokoni hapo,hali ambayao ni hatari kwa maisha ya wananchi wanaofanya shughuli zao katika soko hilo,Lakini usalama wa kinachouzwa hapo.Mwenyekiti wa soko hilo Hassan Baruti ameiambia malunde1 blog kuwa manispaa ya Shinyanga ndiyo ya kulaumiwa kwa tatizo hilo kwani mara kwa mara imekuwa ikidai gari la manispaa ni bovu lakini cha kushangaza wakati mwingine gari hilo linaonekana mtaani.Akaongeza kuwa wafanyabiashara wao wanaendelea kulipa ushuru kama kawaida |
|
Jengo jeupe ndiyo choo cha soko,pembeni ghuba la taka,Hapo waliposimama watoto ndiyo kuna karo la maji ya choo yanayotoririka na kuenea sokoni hapo,kamera za waandishi wa habari zilinasa watoto wakiwa wanachezea maji hayo ya chooni.Wananchi waliitupia lawama manispaa ya Shinyanga kwa kuwapuuza kwenda kunyonya hayo maji machafu ambapo maji yanayotokana na shughuli za akina mama ntilie pamoja na choo vyote yanaiingia kwenye karo moja.Pembeni akina mama ntilie wanaendelea kuuza chakula.Je usalama wa afya za binadamu katika eneo hilo upo? Endelea kutafakari.... |
|
Hapo ndipo maji machafu ya CHOO yanapotokea na kuzagaa eneo loa soko la nguzo nane.Kufuatia hali hiyo waandishi wa habari walipiga hodi kwa meya wa manispaa ya Shinyanga,ambaye ni diwani wa kata ya Shinyanga mjini lilipo soko hilo Gulam Hafeez Mukadam,ambapo alisema manispaa ya Shinyanga inakabiliwa na tatizo la gari la kubebea maji taka na kwamba gari lililopo ni MOJA pekee na limeharibika na lipo kwenye matengenezo likitengemaa wiki hii maji hayo yatatolewa |
|
Hapa ni katika eneo la Machinjioaya ng'ombe katika eneo la Nguzo nane mjini Shinyanga,maji machafu yanayotokana na shughuli nzima ya uchinjaji ,vikiwemo vinyesi vya ng'ombe yakiwa eneo hilo nyeti.Maji hayo pia yamelalamikiwa na wakazi wa eneo hilo kwani yamekuwa yakitiririka hadi kwenye makazi yao,sehemu za biashara zao n.k UTAONA PICHA HAPO CHINI. |
|
Ni katika eneo la machinjio ya Nguzo nane mjini Shinyanga,maji machafu yakiwa yametawala,Je nyama inayotoka hapo iko salama?,endelea kutafakari..... |
|
Harakati za kunusuru afya za wananchi ndiyo hizo zinaendelea,ujenzi wa karo kwa ajili ya kuhifadhi maji machafu yanayotoka katika eneo la machinjio hayo unaendelea,ambapo kwa mujibu wa mstahiki meya wa manispaa ya Shinyanga Gulam Hafeez Mukadam alisema mkakati uliopo hivi sasa ni kukarabati machinjio yote yaliyopo katika manispaa ya Shinyanga |
|
Huo ndiyo mtaro unaotoa maji machafu kutoka eneo la machinjio ya nguzo nane ,na maji hayo yenye kinyesi cha ng'ombe yamekuwa yakisambaa kwenye maeneo yanayozunguka eneo la machinjio |
|
Maji hayo machafu yanapita katika eneo hilo nyeti la kuuzia unga wa ugali(Shinyanga Food Enterprises) |
|
Kijana anauza mahindi ya kuchoma,nyuma yake kuna mfereji unaopitisha maji machafu yanayotoka katika machinjio ya nguzo nane |
|
Maji hayo machafu huishia kwenye mashamba ya wakazi wa eneo hilo linalojulikana kama mtaa wa Viwandani |
|
Hapa ni katika eneo la mtaa wa Viwandani.
Hiyo ndiyo hali halisi ambayo ipo katikati ya mji wa Shinyanga.Ziara ya waandishi wa habari kuangalia mazingira ya mkoa wa Shinyanga ,amkoa ambao una kila aina ya utajiri na sasa viwanda vya kila aina vinaendelea kujengwa katika mkoa huu ambao kimaendeleo umekuwa nyuma sana ukilinganisha na utajiri wake. |
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com