Kijana Sanane Machimi akiwa mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Tabora muda mfupi baada ya kuhukumiwa kifungo cha mwaka mmoja kufuatia kosa la mauaji ya bila kukusudia. |
Mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi
mkoa wa Tabora imemuhukumu kutumikia kifungo cha mwaka mmoja Jela kijana anayefahamika kwa jina la
Sanane Machimi baada ya
kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia.
Akisoma maelezo ya
kosa mbele ya mahakama hiyo,Mwanasheria
upande wa Jamhuri Bw.Nestory Paschal
aliieleza mahakama hiyo kuwa mshtakiwa
Sanane Machimi akiwa na umri wa
miaka 17 mnamo tarehe
7 mwezi wa 5 mwaka 2012 alimuua
bila kukusudia mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la Kweji Ntuvilo kwa kumpiga kwa fimbo kichwani na
ubavuni baada ya kumfumania anafanya
mapenzi na mkewe eneo la vichakani
huko wilayani Sikonge.
Mshtakiwa
alikiri kutenda kosa
hilo kinyume na kifungu namba
195 kanuni ya adhabu sura namba 16
marejeo ya sheria ya
mwaka 2002 ambapo alieleza kuwa
baada ya kumkuta
marehemu akifanya tendo la
zinaa na mkewe haikuwa
rahisi kwake kuvumilia
kitendo hicho na hivyo kushikwa
na ghadhabu ya
kumshambulia hali iliyosababisha
kifo cha marehemu Kweji Ntuvilo aliyekuwa na umri wa miaka 30.
Akisoma hukumu baada
ya kusikiliza maelezo ya pande zote mbili, hakimu
mkazi mwandamizi mwenye mamlaka ya ziada Bw.Thomas Simba
alisema mahakama hiyo tukufu imepitia kwa makini shitaka hilo na kumtia
hatiani Sanane Machimi ambapo alimhukumu kutumikia kifungo
cha kwenda Jela kwa muda wa mwaka mmoja
ili iwe fundisho kwa mtu mwingine atakayediriki kufanya kosa kama hilo.
Hata hivyo mshtakiwa mara
baada ya kusomewa
adhabu hiyo alisikika akimshukuru Mwenyezimungu
akidai kuwa adhabu aliyoipata imekuwa na nafuu sana kwake
kwakuwa
tayari alikuwa amekaa
mahabusu tangu mnamo
mwaka 2012.
Credit-kapipij blog