Uongozi
na wananchi wa Kijiji cha Olgilai, wilayani Arumeru jijini Arusha
umekubaliana kuwachapa viboko hadharani wanawake watakaovaa mavazi ya
nusu uchi hasa vimini na vijana wa kiume wanaovaa suruali chini ya
makalio ‘kata kei’.
Pamoja
na hilo la mavazi, adhabu ya aina hiyo itawakumba pia wanafunzi
watakaopata mimba au kuozeshwa na kuacha masomo wakiwa na umri mdogo,
lengo likiwa ni kukomesha tabia hizo kwa vile zimekithiri kijijini
hapo.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Olgilai, Godson Boazi katika barua yake ya Januari 24, mwaka huu kwa viongozi wa makanisa kijijini hapo, aliwaomba kuunga mkono hatua hiyo katika kurekebisha tabia ndani ya jamii yao.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Olgilai, Godson Boazi katika barua yake ya Januari 24, mwaka huu kwa viongozi wa makanisa kijijini hapo, aliwaomba kuunga mkono hatua hiyo katika kurekebisha tabia ndani ya jamii yao.
“Viongozi
wa dini tunafahamu kazi kubwa ya kutunza kundi la Mungu likae kwenye
maadili mema. Hivyo basi tunaomba mtusaidie jukumu hili ambalo
tumeambatanisha kwenu kwa barua,” ilieleza sehemu ya barua hiyo.
Barua hiyo inaendelea kueleza:
“Vijana wa kiume wanaovaa mlegezo, uendeshaji ovyo wa pikipiki, wavuta bangi, watumiaji wa madawa ya kulevya, wanywa gongo na viroba, uchezaji kamari na karata. Wanaotukana ovyo barabarani na kupiga kelele za uvunjaji wa amani, wezi wa vitu vikubwa na vidogo kama kuku, ndizi, viazi, mahindi na mboga mashambani watashughulikiwa.”Wanakijiji wote wamefurahishwa na kitendo hicho na kwa kauli moja wamepitisha azimio hilo ili kujenga kijiji chenye nidhamu na amani tofauti na hali ilivyo hivi sasa.