Pichani ni baadhi ya wakazi wa Morogoro ambao leo asubuhi walilazimika kutumia usafiri wa vyombo visivyo rasmi kusafirisha abiria, ili kuwahi makazini |
Habari kutoka Morogoro zinasema kuwa wamiliki wa daladala katika Manispaa ya
Morogoro wamesitisha kutoa huduma ya usafirishaji abiria ndani na
Manispaa kwa kile kinachodaiwa kutozwa faini kubwa na askari wa usalama
barabarani pindi magari hayo yanapokamatwa kwa makosa mbalimbali ambapo
kwa wiki hudai hukamatwa mara mbili mpaka tatu huku kiwango cha faini
hiyo kikitajwa kuwa ni kati ya sh30,000 hadi sh120,000 ikiwa kosa moja
ni sh30,000.
Social Plugin