Paroko wa Kanisa la Orthodox, Parokia za Nyamihuu Kalenga, Iringa,
Costantino Mbilinyi akizungunza na waandishi wa habari nyumbani kwake
katika Kijiji cha Nyamihuu jana kuhusu kushambuliwa kwake Kalenga.
Padri
wa Makanisa ya Orthodox katika Kijiji cha Nyamihuu, Kata ya Nzihi,
jimboni Kalenga Constantino Mbilinyi (36) amepigwa na kujeruhiwa na watu
wanaodaiwa kuwa ni wafuasi wa CCM.
Baada ya kukutwa na mkasa huo, Padri
Mbilinyi alishikiliwa kwa muda katika Ofisi ya Ofisa Mtendaji wa kijiji
hicho, Kumbusho Chengula, na baadaye alichukuliwa na askari ambao
walimpeleka Kituo cha Polisi Kati, mjini Iringa kwa mahojiano.
Kasisi
huyo akizungumza na waandishi wa habari jana alisema alipatwa na mkasa
huo alipoambatana na viongozi wa Chadema waliopiga kambi kwenye Kata ya
Nzihi, ambao walikuwa wakielekea kwenye mikutano ya kampeni za kumnadi
mgombea ubunge kupitia chama hicho, Grace Tendega.
Alisema viongozi hao walimwomba awasindikize kwenda Kijiji cha Igangimali kwa ajili ya kumwona mtu aitwaye, Samti Ngonjela ili wamkabidhi mabango Tendega.
Alisema viongozi hao walimwomba awasindikize kwenda Kijiji cha Igangimali kwa ajili ya kumwona mtu aitwaye, Samti Ngonjela ili wamkabidhi mabango Tendega.
“Waliniomba na mimi nikakubali kwa kuwa
nilikuwa na ratiba ya kwenda katika kijiji kile kumwona Bento Ngaila
ambaye tulitaka kuzungumza kuhusiana na mchakato wa shamba langu
lililoko katika kijiji kile,” alisema Mbilinyi na kuongeza:
“Tulipofika
nilimtafuta Ngonjela kwa ajili ya kuwaonyesha viongozi wa Chadema,
lakini wakati huo vijana wengine wa Chadema walianza kubandika mabango
ya mgombea katika klabu ya pombe ya Lazaro Nzigi, na ghafla lilitokea
kundi la wanachama wa CCM na kuanza kuwafukuza.”
Alisema vijana hao walimgeukia wakimshutumu kwamba aliwapeleka watu wa Chadema katika eneo lile ambalo wao walikuwa na mkutano wa ndani.
Mbilinyi alisema licha ya kujitetea, wafuasi hao wa CCM walimkamata na
kumwangusha na kumfunga mikono nyuma kwa kamba ya katani.
Wakati huo
wafuasi wa Chadema walikuwa wameshaondoka. “Walianza kunipiga na
kunisukuma hali iliyonifanya nianguke chini na kuumia mkononi na
mgongoni.
Nikiwa nimeanguka chini na mikono yangu imefungwa kamba kwa
nyuma mmoja wa vijana hao alichukua pilipili na kuingiza kwenye mfuko wa
shati langu kisha wakanichukua na kunipeleka ofisi ya ofisa mtendaji
iliyoko Nyamihuu,” alisema Mbilinyi.
Mbilinyi alisema makada hao wa CCM walimweleza ofisa huyo kwamba
alikwenda na wenzake kuwafanyia fujo na kwamba aliwatukana na kuwatishia
maisha. Alisema watu waliomfanyia unyama huo anawafahamu.
Ofisa Mtendaji
Kaimu Ofisa Mtendaji, Chengula alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa alilazimika kumweka ndani kwa kuhofia hali ya usalama.
Ofisa Mtendaji
Kaimu Ofisa Mtendaji, Chengula alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa alilazimika kumweka ndani kwa kuhofia hali ya usalama.
“Ni
kweli....nilipigiwa simu na kada wa CCM ninayemfahamu akaniambia Padri
huyo amepeleka wanachama wa Chadema kwenye eneo ambalo wao walikwenda
kuwatembelea wanachama wao na kwamba waliwatukana,” alisema Chengula na
kuongeza:
“Ilipofika saa 12 jioni niliona kundi la watu wakija ofisini
huku wakiwa wamemtanguliza Mbilinyi ambaye alikuwa amefungwa kamba
mikononi.”
Alisema baada ya kupokea maelezo ya makada wa CCM aliamuru
Padri Mbilinyi afanyiwe upekuzi kisha alimweka ndani lakini baadaye saa 5
usiku polisi wakiongozana na viongozi wa Chadema na CCM walifika kisha
kuondoka naye.
CHADEMA, CCM
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo ya Ufundi, Benson Kigaila alisema alikwenda polisi kumwekea dhamana. Aliwapongeza polisi kwa kufika haraka Kata ya Nyamihuu ambako ndiko alikokamatwa padri huyo na kupigwa. Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Iringa, Delfina Mtavilalo alisema:
CHADEMA, CCM
Mkurugenzi wa Oganaizesheni na Mafunzo ya Ufundi, Benson Kigaila alisema alikwenda polisi kumwekea dhamana. Aliwapongeza polisi kwa kufika haraka Kata ya Nyamihuu ambako ndiko alikokamatwa padri huyo na kupigwa. Mwenyekiti wa CCM, Wilaya ya Iringa, Delfina Mtavilalo alisema:
“Huyo
padri ninamfahamu lakini taarifa kwamba alipigwa na wafuasi wa CCM
hazina ukweli wowote.” Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Ramadhan
Mungi hakupatikana jana kuzungumzia tukio hilo na simu yake ilikuwa
ikiita bila kupokelewa.
Chanzo- zeangazio blog