CCM YAPATA PIGO KIFO CHA KADA WAKE MAARUFU MKOANI SHINYANGA
Thursday, March 20, 2014
Chama
Cha Mapinduzi mkoani Shinyanga kimepata
pigo Kufuatia kifo cha mmoja wa makada wake maarufu ambaye pia alikuwa
mwenyekiti wa CCM katika kata ya Iselamagazi wilayani Shinyanga, Paul Zephania
(61) aliyefariki dunia juzi baada ya kuugua malaria tarehe 14 mwezi huu na
kufariki tarehe 18 mwezi huu saa 12 jioni.
Kwa
mujibu wa taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa CCM mkoani Shinyanga, Khamis
Mgeja amesema CCM itamkumbuka Zephania kwa juhudi zake za uimarishaji wa chama alizokuwa
akizifanya wakati wa uhai wake na kwamba
ameacha pengo kubwa mbalo litachukua muda kuzibika
kutokana na shughuli alizokuwa akizifanya ndani ya chama.
Akiongoza
mazishi ya kada huyo kijijini kwake Iselamagazi jana, Mgeja alisema
marehemu Zephania alijiunga na chama cha mapinduzi tangu mwaka 1978 na mwaka 2002
alikuwa katibu wa tawi CCM wilayani humo, na mnamo mwaka 2012
alikuwa mwenyekiti wa kata ya Iselamagazi hadi mauti kumfika.
Alisema CCM
imepata pigo kubwa kwa kuondokewa na kiongozi
wetu shupavu ambaye amekitumikia Chama kwa mda mrefu sana (36),tangu ajiunge na
CCM alikuwa mchapa kazi na haja wahi kulalamikiwa na mtu yeyote na ndio maana
mnaona maelfu ya watu Mmekuja kumpumzisha kwenye makazi yake ya milele kwa
sababu alikuwa mtu wa watu.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin