|
Ni katika viwanja vya mahakama ya mwanzo Nguzo nane mjini Shinyanga ambako jioni ya leo kumefanyika mkutano mkubwa wa chama cha demokrasia na maendeleo CHADEMA na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa mkoa wa Shinyanga.Pichani ni miongoni mwa waliotangaza nia kugombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini ndani ya CHADEMA Francis Kasili akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema CHADEMA siku zote itahakikisha inampigania mnyonge ambaye CCM imeshindwa kumtatulia matatizo yake.
|
|
Mwenyekiti wa vijana CHADEMA wilaya ya Shinyanga mjini Hassan Baruti akizungumza katika mkutano wa chama hicho jioni ya leo mjini Shinyanga ambapo alisema watanzania wana matumaini na Chadema ndiyo maana hata kwenye mikutano ya chadema wanahudhuria kwa wingi bila kubebwa kwenye magari kama wanavyofanya CCM kwenye mikutano yao na kuwataka watanzania kuendelea kuipa nguvu Chadema ili kuhakikisha kuwa Shinyanga inakuwa mikononi mwa chadema. |
|
Mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Shinyanga mjini Siri Yasin akiwahutubia wakazi wa Shinyanga ambapo alisema CHADEMA ni chama kiongozi tofauti na CCM chama kinachotawala watanzania na kuwasababishia matatizo mbalimbali huku wachache wakitumia CCM kujinufaisha wenyewe kwa kurithishana madaraka kijanja kijanja kama inavyofanyika sasa katika jimbo la Chalinze na Kalenga ambako watoto wa wakubwa ndiyo wanagombea kupitia CCM ili kuendelea kuwanyonya watanzania |
|
Kulia ni aliyekuwa diwani wa Kata ya Ngokolo katika manispaa ya Shinyanga kupitia CCM (2005/2010) Saganda Khalid Saganda ambaye sasa amejiunga CHADEMA,akikaribishwa katika jukwaa na katibu wa chadema mkoa wa Shinyanga Nyangaki Shilungushela(kushoto) mzee wa Utaratibu.Saganda Khalid Saganda alisema ameamua kuhamia CHADEMA kwani ndiyo chama kinachotetea maslahi ya kila mtanzania.Alisema wakati wa uongozi wake katika kata ya Ngokolo mwaka 2005/2010 alikuwa CCM kimwili lakini Roho yake haikuwa CCM huku akiwataka watanzania kuwapuuza wale madiwani waliohamia CCM hivi karibuni(Sebastian Peter maarufu kwa jina la Obama na Zacharia Mfuko) kwani wameshawishiwa na CCM na kuisaliti Chadema kwa tamaa ya pesa. |
|
Wakazi wa mkoa wa Shinyanga wakiwa katika eneo la mkutano wakifuatilia mkutano wa chadema na hapa wanafurahia majina mapya ya waliokuwa madiwani wa CHADEMA waliohamia CCM hivi karibuni.Makamanda wa chadema hivi sasa wamempa jina Sebastian Peter maarufu kwa jina Obama aliyekuwa diwani wa Ngokolo kuwa OMAMA badala ya Obama na Zacharia Mfuko aliyekuwa diwani wa kata ya Masekelo katika manispaa ya Shinyanga kuitwa MFUGO badala ya Mfuko |
|
Mkutano unaendelea wananchi wakisikiliza kwa umakini zaidi kilichokuwa kinajiri ndani ya viwanja vya mahakama ya mwanzo nguzo nane mjini Shinyanga |
|
Mjumbe wa kamati ya uhamasishaji CHADEMA kanda ya ziwa mashariki Peter Machanga akiwahutubia wakazi wa Shinyanga jioni ya leo ambapo alisema madiwani wa CHADEMA waliohamia CCM katika manispaa ya Shinyanga walipewa milioni 20 na kuongeza kuwa cheki walizopewa ni feki na sasa wanajuta kuhamia CCM.Aliongeza kuwa Sebastian Peter na mwenzake wana laana kubwa kwani wakati wanahamia CCM hakuna mwanachadema yeyote aliyewasindikiza,walihama peke yao |
|
Mwenyekiti wa rasilimali CHADEMA kanda ya ziwa mashariki Emmanuel Mbise akizungumza katika mkutano wa chadema ambapo alisema mbunge wa jimbo la shinyanga mjini Stephem Masele ni kama mbunge wa kuteuliwa na sasa ameanza kuhonga watanzania.Akihutubia maelfu ya wananchi leo alisema hivi sasa aliyekuwa anajiita Obama wa Ngokolo sasa ni vyema wakamwita OMAMA na Zacharia Mfuko kumwita MFUGO kwani hivi sasa amekuwa mfugo wa CCM kwa tamaa ya pesa walizohongwa na mbunge Shinyanga mjini ili wasaliti chama. |
|
Mwenyekiti wa kamati ya uenezi na uhamasishaji CHADEMA kanda ya ziwa mashariki,ambaye pia ni ,mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kahama mkoa wa Shinyanga Juma Protas Ntahimpera akiwahutubia wakazi wa shinyanga ambapo pamoja na mambo mengine aliwaomba radhi wakazi wa Shinyanga kutokana na viongozi wa CHADEMA waliopaswa kuja Shinyanga kuongea na wananchi kutofika katika eneo la mkutano ambapo alisema wanahudhuria Dodoma kwa ajili ya kupiga kura ya siri bungeni leo.Viongozi waliotakiwa kuwepo Shinyanga ni Ezekiel Wenje mbunge wa Mwanza mjini,Joseph Mbilinyi mbunge wa Mbeya mjini, Sylivester Kasulumbayi Maswa Mashariki na Godbless Lema wa Arusha mjini |
|
Mwenyekiti wa vijana CHADEMA mkoa wa Shinyanga Renatus Nzemo akiwasalimia wananchi wa mkoa wa Shinyanga waliojitokeza kwa wingi katika mkutano huo leo |
|
Wananchi wakimsikiliza mwenyekiti wa kamati ya uenezi na uhamasishaji CHADEMA kanda ya ziwa
mashariki,ambaye pia ni ,mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kahama mkoa wa
Shinyanga Juma Protas Ntahimpera |
Mwenyekiti wa kamati ya uenezi na uhamasishaji CHADEMA kanda ya ziwa
mashariki,ambaye pia ni ,mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kahama mkoa wa
Shinyanga Juma Protas Ntahimpera alisema CCM hivi sasa inatumia wajumbe wake kwenye bunge la katiba ili kukataa serikali tatu.Aliongeza kuwa viongozi wa chadema walipaswa kuwepo shinyanga leo na badala yake sasa watakuja Shinyanga mjini mara baada ya kutoka jimbo la Kalenga Iringa.
|
Wananchi wakifuatilia mkutano ambapo Mwenyekiti huyo wa kamati ya uenezi na uhamasishaji CHADEMA kanda ya ziwa
mashariki,ambaye pia ni ,mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kahama mkoa wa
Shinyanga Juma Protas Ntahimpera alimshangaa aliyekuwa diwani wa kata ya Ngokolo Sebastian Peter kuwahadaa watanzania kuwa aliyekuwa mgombea wa jimbo la Shinyanga mjini kupitia CHADEMA marehemu Philip Shelembi kwamba aliuliwa na Freeman Mbowe wakati inajulikana wazi kwamba Mbunge wa jimbo la Shinyanga mjini kupitia CCM ndiye mhusika na kwamba hata ubunge wake sio halali kwani alichakachua kura na matokeo yake akatangazwa kuwa mshindi katika uchaguzi wa mwaka 2010 kwa kumzidi mgombea wa CHADEMA kura moja |
|
Mkutano unaendelea,Jukwaa kuu wakimsikiliza kwa umakini zaidi Mwenyekiti huyo wa kamati ya uenezi na uhamasishaji CHADEMA kanda ya ziwa
mashariki,ambaye pia ni ,mwenyekiti wa CHADEMA wilaya ya Kahama mkoa wa
Shinyanga Juma Protas Ntahimpera ambapo pamoja na mambo mengine aliliomba jeshi la polisi kutenda haki katika kuwatumikia watanzania lakini pia kuiunga mkono CHADEMA kwani ndiyo chama kitakachoshika dola mwaka 2015.Aliongeza kuwa CHADEMA haitarudi nyuma hivyo wananchi waendelee kuiamini kwani ndiyo mkombozi wao. |
|
Wakazi wa shinyanga wakifuatilia mkutano wa Chadema,wengine walisitisha kwa muda kufanya biashara zao na kuhudhuria mkutano huo kama unavyoona hapo kwenye picha |
|
Ni katika eneo la mkutano viwanja vya Mahakama nguzo nane mjini Shinyanga jioni ya leo |
|
Katika kujenga chama watu wenye mapenzi mema na CHADEMA walichangia kile walichokuwa nacho mfukoni ili kufanikisha mpango wa chama hicho kununua vifaa vya matangazo ambapo shilingi milioni mbili zinahitajika na leo zimepatikana shilingi laki 3 na elfu ishirini.
ENDELEA KUTAZAMA MATUKIO KATIKA PICHA
|
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com