Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Chadema wafunika Shinyanga!!! WASHAMBULIA JUKWAA KWA ZAMU,FUATILIA HAPA MKUTANO WAO MJINI SHINYANGA MWANZO MWISHO

Ni katika viwanja vya mahakama ya mwanzo Nguzo 8 mjini Shinyanga jioni ya leo wakati wa mkutano wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ambako madiwani 6 wa Chama hicho katika manispaa wamekusanya mamia ya watu katika mkutano huo ,ambapo baadhi ya wakazi wa Shinyanga wameuita mkutano wa Kujibu mashambulizi ya CCM ambapo Februari 25 mwaka huu, katibu wa siasa na uenezi ccm taifa Nape Nnauye alifika katika eneo hilo na kufanya mkutano wa hadhara na waliokuwa madiwani wa CHADEMA Sebastian Peter na Zacharia Mfuko wakajiunga na ccm na kuchoma kombati zao hadharani

Aliyesimama ni mwenyekiti wa Vijana CHADEMA mkoa wa Shinyanga Hassan Baruti akizungumza katika mkutano huo ambapo amesema CCM hata ingetumia pesa kiasi gani kununua wanachadema kamwe hawatarudi nyuma kwani chama chao kinalenga kutetea na  kuwakomboa wanyonge huku akiwaomba wanashinyanga kumpuuza mbunge wa Shinyanga mjini anayetumia pesa vibaya kwa kuhonga watu badala ya kuwaletea maendeleo mfano kununua hata dawa katika hospitali
Diwani wa kata ya Ibadakuli  katika manispaa ya Shinyanga bwana Leonard Mayunga akizungumza  katika mkutano huo ambapo alisema Sebastiani Peter  walishawishiwa na mbunge wa jimbo la Shinyanga Mjini Stephen Masele ili wahamie CCM kwa  kupewa milioni 15 kila mmoja na kuamua kuhamia CCM.Diwani huyo alisema wananchama wa Chadema waliohamia CCM wamehama kutokana na tamaa ya pesa huku akisisitiza kuwa yeye atakuwa wa mwisho kushawishiwa na ccm na kuwataka wananchi kuendelea kuiamini CHADEMA





Wakazi wa mkoa wa Shinyanga wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika mkutano huo ambapo makamanda wa Chadema waliwaomba wananchi kuwapuuza wanaohamia CCM kwa tamaa ya pesa na kwamba madiwani hao tayari walikuwa mizigo katika chama hivyo kitendo cha kuhamia CCM ni kama kujihami tu
Diwani wa viti maalum kutoka kata ya Masekelo bi Zainabu  Mohamed Kheri  wa CHADEMA akizungumza katika mkutano wa leo jioni ambapo aliwataka wakazi wa Masekelo kutosikitika wala kusononeka hivyo wawe wavumilivu  kwani tayari kata ya Masekelo ina Diwani wa Chadema(YEYE) hivyo ataisimamia kata hiyo katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Masekelo.Diwani huyo wa viti maalum alitumia fursa hiyo kuwatahadhalisha wananchi kuhusu mpango wa CCM wa kununua shahada za kupigia kura huku akisisitiza kuwa CHADEMA ni Mpango wa Mungu hivyo hawatarudi nyuma katika kuwakomboa watanzania
Diwani wa kata ya Kitangiri katika manispaa ya Shinyanga,George Musaa Kitalama akizungumza katika mkutano wa CHADEMA leo mjini Shinyanga ambapo alisema yeye ni miongoni mwa madiwani walioshawishiwa na Mbunge wa Shinyanga mjini Stephen Masele ili ahamie CCM lakini akagoma.Aidha kitalama alisema Mbunge wa Shinyanga mjini Stephem Masele hajafanya lolote katika jimbo lake badala yake anaazima watu kutoka nje ya mkoa kumsaidia kuongea kwenye mikutano na sasa ameanza kununua watu

Mwenyekiti wa chadema wilaya ya Shinynga mjini bi Siri Yasin akizungumza katika mkutano huo ambapo aliwataka watanzania kuendelea kuipa nguvu Chadema na kwamba wataendelea kusonga mbele katika mapambano yao dhidi ya CCM.Siri Yasin atasimamia kata ya Ngokolo iliyoachwa na Sebastian Peter ambaye amehamia CCM.
Wananchi wakifuatilia mkutano wa Chadema,ambapo mashambulizi ya makamanda wa chadema waliyalekeza zaidi kwa mbunge wa Shinyanga mjini kupitia CCm ambaye walisema amekuwa akihubiri kuwa madiwani wa Chadema katika jimbo lake ni mzigo kwamba wanarudisha nyuma harakati za ccm

Katibu wa chadema mkoa wa Shinyanga Nyangaki Shilungushela maarufu kwa jina la "Mzee wa Utaratibu"akizungumza jioni ya leo ambapo alisema wale madiwani wa chadema waliojiunga CCM walikuwa mizigo ndani ya chama na kwamba ana uhakika ndani ya wiki mbili zijazo ccm italalamika kwa kupokea madiwani mizigo.Shilungushela amewataka  wananchi kushirikiana na chadema katika kuing'oa ccm katika manispaa ya Shinyanga na mkoa kwa ujumla huku akiongeza kuwa mambo yanayofanywa na ccm hivi sasa ya kurubuni viongozi wa Chadema ni "Sawa na kuangusha mbuyu kwa kutumia wembe"

Mkutano unaendelea,wananchi wakisikiliza kwa umakini kilichokuwa kinasemwa na katibu wa chadema mkoa wa Shinyanga Nyangaki Shilungushela

Ni katika eneo la mkutano wa chadema leo jioni mjini Shinyanga,ambako mamia ya wakazi wamejitokeza kusikiliza yaliyokuwa yanajiri kwenye mkutano

Wapo waliokfika eneo la mkutano na baiskeli zao wanazozitumia kusafirishia abiria maarufu daladala,walisitisha kazi yao na kuamua kwenda kwenye mkutano wa chadema wakiamini pengine chama hicho kinaweza kuwaletea kile wanachokihitaji

Diwani wa kata ya Ndala bwana George Sungura Kidosi akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema chadema itahakikisha inarudisha kata za Masekelo na Ngokolo kwenye mikono ya chadema.Sungura pia alisema wananchi wa shinyanga wasikate tamaa kwani waliohama chadema ndiyo wamechochea kasi ya mapambano katika kuiondoa ccm madarakani
Wananchi wanasikiliza kilichokuwa kinajiri katika viwanja vya mahakama ya mwanzo kwenye mkutano wa Chadema,wamo pia waandishi wa habari  kama huyo bwana mwenye tisheti iliyoandikwa ZIRO( Faustine Kasala kutoka radio Faraja fm stereo ya mjini Shinyanga) wa tatu kulia liyevaa kofia ni mwandishi mkongwe wa habari hapa nchini bwana Anikaz Ndaji Kumbemba

Viongozi wa chadema na wananchi wakifuatilia mkutano
Baada ya mkutano madiwani wa CHADEMA na wananchi  walifanya changizo kwa ajili ya kununua vifaa vya matangazo ambapo shilingi laki moja na elfu 57 zilipatikana.
 Baada ya mkutano kumalizika kila mtu anawaza yake,waandishi wa habari wakiwa eneo la tukio,wa kwanza ni Bi Veronica Natalis,wa pili mwenye air phone ni bwana Steve Kanyefu wote kutoka radio faraja ya mjini Shinyanga,mwingine ni bwana Michael mdau wa maendeleo Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com