Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’.
IMEBAINIKA kuwa ndani ya tasnia ya filamu Bongo kuna
baadhi ya wasanii wanaofanya mapenzi ya jinsia moja yaani mashoga,
Risasi Mchanganyiko limenyetishwa.
Hilo limeibuka ikiwa ni siku chache baada ya Rais wa Uganda, Yoweri
Museven, kupitisha sheria nchini mwake ya kupiga marufuku mavazi yasiyo
na staha, uvunjifu wa maadili na mapenzi ya jinsia moja.
Uganda ipo katika Jumuiya ya Afrika Mashariki ikiunganishwa na nchi za Tanzania, Kenya, Rwanda, Burundi na Uganda yenyewe.
HABARI KAMILI
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vilivyomo ndani ya kundi hilo, baadhi ya wasanii wa kiume wanadaiwa kuwa ni mashoga, ingawa wanajifanya vidume vya mbegu.
Kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali vilivyomo ndani ya kundi hilo, baadhi ya wasanii wa kiume wanadaiwa kuwa ni mashoga, ingawa wanajifanya vidume vya mbegu.
“Wapo mashoga na mabwana zao tunawajua ila sema sasa kwa sababu huna
ushahidi wa moja kwa moja na hujamfuma kwenye tukio, unashindwa
kumtaja,” alisema msanii mmoja wa kike, Bongo.
“Yule…(analitaja jina la msanii mkubwa) bwana’ke alifariki na sasa
ana mwingine lakini ndani ya Bongo Muvi anaonekana kiwembe kwa sababu
ana msururu wa wanawake,” alisema.
AMSHAURI JK
“Ingekuwa vyema sana kama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akafanya kama alivyofanya mwenzake wa Uganda, Yoweri Museven katika kupiga vita ushoga,” alipendekeza msanii huyo.
“Ingekuwa vyema sana kama Rais Jakaya Mrisho Kikwete akafanya kama alivyofanya mwenzake wa Uganda, Yoweri Museven katika kupiga vita ushoga,” alipendekeza msanii huyo.
Msanii mwingine wa kike ambaye amekuwa kwenye tasnia hiyo tangu enzi za
makundi ya sanaa kutamba runingani (jina kapuni) naye alikiri kuwepo
kwa ishu hiyo lakini akadai wanafanya kwa siri sana.
“Kuna wasanii
wanaonekana watanashati mbele ya jamii lakini ni chakula ya watu kwa
kuwa wanapenda sana vitu vya bure,” alisema msanii huyo na kuongeza:
“Wapo wengi tu ndiyo maana katika maisha yangu sijawahi kutoka na
mwanaume wa Bongo Muvi, ni wachafu sana.
Siku zote wasanii wa kike ndiyo
tunaoambiwa kuwa ni malaya, eti tuna tamaa na habari nyingi
zinatuchafua siye lakini ukweli ni kwamba hata wanaume wana tamaa ya
maisha mazuri na mwishowe wanageuzwa wanawake.”
HUYU YUPO TOFAUTI NA WENZAKE
“Sikia nikuambie, ni kweli hili suala lipo lakini si kwa wote na kuna baadhi huwa wanasingiziwa tu. Unajua nini? Unaweza kukuta mtu ana tabia tu ya kujipenda, lakini wengine wanasingizia kuwa eti ni mashoga – siyo kweli.

“Mfano hata uje na greda hapa, akitokea mtu anazungumza upuuzi eti
JB, Dk. Cheni, Ray, Hemed PHD, Mlela au Dude ni mashoga, nitabishana nao
mpaka mwisho.
Hao ni watu ambao wanajipenda tu, sasa ukiwahusisha na
huo ujinga nitashangaa sana. Sisemi kuwa wanatajwa ila sasa akitokea
mjinga akaja na hoja hiyo, nitabishana naye,” alisema msanii mmoja ndani
ya Bongo Muvi.
Msanii Hisani Muya ‘Tino’ aliwahi kuigiza kama shoga na kusababisha
minong’ono kwenye jamii, katika filamu aliyoipa jina la Shoga lakini
ilizuiwa na serikali.
Mwingine ni Dk. Cheni ambaye amecheza kama shoga kwenye filamu yake ya Nimekubali Kuolewa, ingawa bado haijatoka mpaka sasa.
Msanii huyo akizungumzia hayo, alisema: “Kucheza filamu kama shoga
hakuna maana kuwa kweli ni shoga, ni kuvaa uhusika tu.
Watu
wasiwahusishe wasanii walioigiza kama mashoga kwenye hii skendo,”
aliweka nukta msanii huyo mwenye maneno mengi.
WASIKIE WENYEWE
Baada ya kupata taarifa hizo, waandishi wetu waliwatafuta baadhi ya wasanii wa kiume Bongo wanaotesa na kuwauliza kuhusu ishu hiyo (wasanii hao hawamo kwenye orodha tuliyonayo). Wa kwanza kuzungumza alikuwa ni Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni ambaye alisema:

“Miye sina la kusema kuhusu hilo, ni vyema
kama utamtafuta mwenyekiti (Bongo Movie Unity, Steve Nyerere) ndiye
mwenye mamlaka ya kuzungumza masuala kama hayo.”
KULWA KIKUMBA ‘DUDE’
“Hilo suala la ushoga ndani ya Bongo Muvi lipo hata miye nalisikiasikia, lakini halina uthibitisho ila kusemwa linasemwa sana.” STEVE NYERERE Mwenyekiti wa Bongo Movie Unity, Steven Mengere ‘Steve Nyerere’:
“Ni
kweli taarifa hizo zipo, wasanii wakishakunywa pombe huwa wanafanya
mambo ya ajabu sana kuashiria tabia zao halisi, mimi kama mwenyekiti wa
Bongo Movie huwa ninaumia sana.
“Nitahakikisha nawafukuza mashoga wote hata kama tutabaki wawili katika kundi letu, bora wawe na heshima.”
MWAKIFWAMBA SASA
Rais wa Shirikisho la
Filamu Tanzania ‘TAFF’, Simon Mwakifwamba: “Hiyo ishu ni kweli ipo,
ndani ya Bongo Muvi, mashoga wapo wengi sana, ila bado hatujapata
ushahidi wa kuweza kuwataka hadharani.”
credit-gpl