Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

FUATILIA HAPA KILICHOJIRI SHINYANGA LEO,KIKAO CHA KAMATI YA USHAURI MKOA ,WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS UTAWALA BORA GEORGE MKUCHIKA AHUDHURIA PIA



Awali mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga akifungua kikao cha kawaida cha 25 cha kamati ya Ushauri ya mkoa akimkaribisha katika kikao hicho waziri wa nchi ofisi ya rais utawala bora inayohusika na masuala ya rushwa na maadili ya viongozi  George Mkuchika ili awasilishe
mada juu ya utawala bora kwenye kikao cha kamati ya ushauri kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga.

Waziri wa nchi ofisi ya rais utawala bora inayohusika na masuala ya rushwa na maadili ya viongozi  George Mkuchika wakati akiwasilisha mada juu ya utawala bora kwenye kikao cha kamati ya ushauri kilichofanyika katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga ambapo alisema vitendo vya rushwa vinapotawala sehemu za kazi inahatarisha uhai na usalama wa taifa pamoja na kutotimiza utekelezaji wa majukumu ya serikali kwa watumishi wake hivyo kumtaka kila mmoja kuzingatia wajibu wake na kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi.Aidha Mkuchika alisema halmashauri nyingi hapa nchini zinafanya kazi vizuri tatizo ni kwamba hawasemi mafanikio waliyofikia.
Wajumbe mbalimbali wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wakisikiliza kilichokuwa kinazungumzwa na waziri wa nchi ofisi ya rais utawala bora inayohusika na masuala ya rushwa na maadili ya viongozi  George Mkuchika,ambaye alisema vitendo vya rushwa vinapokithiri katika jamii husababisha maovu kuongeza katika jamii na wakati mwingine kusababisha wananchi kukosa imani na serikali yao hali inayopelekea wananchi kujichukulia sheria mkononi kwa mfano vitendo vya mauaji vinavyoendelea katika jamii ambapo vikongwe,albino  na watu mbalimbali wamekuwa wakiuawa kikatili.
Ndani ya ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga mjini Shinyanga kwenye kikao cha kawaida cha 25 cha kamati ya Ushauri ya mkoa ambapo wadau katika sekta mbalimbali wamehudhuria,akiwemo pia waziri wa nchi ofisi ya rais utawala bora inayohusika na masuala ya rushwa na maadili ya viongozi  George Mkuchika .Pichani ni kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Shinyanga Gasto mkono akizungumza katika kikao hicho ikiwa ni sehemu ya mada iliyowasilishwa na Mheshimiwa Mkuchika juu ya utawala Bora.Pamoja na mambo mengine alisema miongoni mwa mambo yanayochangia kuwepo kwa rushwa katika jamii ni wananchi kuwaona watenda rushwa kuwa ni mashujaa huku wengine wakishidwa kutoa ushahidi pindi unapohitajika.Katika hatua nyingine aliwataka viongozi wa halmashauri,madiwani na wabunge kutoa elimu kwa wananchi kuhusu miradi katika maeneo yao kwani hivi wakandarasi wamekuwa wakishirikiana na baadhi ya viongozi kujenga miradi iliyo chini ya viwango.
Wajumbe wa kikao wakifuatilia kilichokuwa kinajiri kwenye kikao hicho cha kamati ya ushauri ya mkoa wa Shinyanga leo katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga,ambako mambo kadha wa kadha yamejadiliwa kuhusu maendeleo ya mkoa wa Shinyanga
Alisimama ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga Khamis Mgeja akichangia mawili matatu katika kikao hicho ambapo aliipongeza serikali ya awamu ya nne kwa  kusimamia mambo mbalimbali ya maendeleo likiwemo suala la kupiga vita rushwa huku akisema pamoja na jitihada za serikali kupiga vita adui Rushwa lakini kila mtu katika jamii ana wajibu wa kupiga vita rushwa.
Wajumbe wakifuatilia kilichokuwa kinajiri kwenye kikao hicho


Aliyesimama ni katibu msaidizi secretariati ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya magharibi -Tabora Salvatory Kilasara akiwasilisha mada kuhusu sheria ya maadili ya viongozi wa umma na majukumu ya sekretariati ya maadili.
Wajumbe wa kikao cha kamati ya ushauri ya mkoa wakimsikiliza katibu msaidizi secretariati ya maadili ya viongozi wa umma kanda ya magharibi -Tabora Salvatory Kilasara wakati akiwasilisha mada kuhusu sheria ya maadili ya viongozi wa umma na majukumu ya sekretariati ya maadili.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com