Ikiwa
ni siku chache baada ya mfungwa wa gereza la Butundwe wilayani Geita
Goefry(19) Emmanuel mwenye namba 224/20013 kutuhumiwa kubaka mwanafunzi
wa darasa la tano mwenye umri wa miaka 15 katika shule ya msingi Luhuha
akiwa na wenzake wakichanja kuni porini ,uchunguzi umebaini kuwepo na
wafungwa wengine walishatoroka gerezani na kutokomea kwenye hifadhi ya
msitu wa Butundwe
Kwa mujibu wa taarifa zilizothibitishwa na mkuu wa magereza mkoa wa Mwanza anayekaimu pia mkoa wa Geita,ni kwamba wafungwa hao walitoroka Machi 6,mwaka huu saa 6 mchana wakiwa kazini chini ya ulinzi wa askari magereza wawili..
Kaimu mkuu wa magereza mkoani Geita,Raphael Mollel alipotafutwa kwa njia ya simu alithibitisha kutoroka kwa wafungwa hao.alisema kuwa,
''Wafungwa walikurupuka na kutokomea kusikojulikana kwenye Msitu ulioko karibu na shamba la gereza,zoezi la kuwafuatilia bado linaendelea'' alisema Mollel kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi(sms) baada ya kupigiwa simu na kudai yuko kwenye kikao.
Hata hivyo alipoulizwa wafungwa hao walitoroka vipi wakiwa chini ya ulinzi wa askari,alisema hana taarifa kamili na kudai kuwa atakuwa na taarifa sahihi akifika eneo la tukio.
Wafungwa hao ni Edson Fitina(24)mkazi wa Chato,Emmanuel Ernest(18)mkazi wa Buseresere wilayani Chato,Safari Moshi(20)mkazi wa Katoro wilayani Geita,na Musa Deusi(22)mkazi wa Nyarugusu wilayani Geita.
Wafungwa hao kwa pamoja walikuwa wakitumikia kifungo cha miaka mitatu jela kwa kosa la kuvunja nyumba na kuiba.
Inadaiwa kuwa
wafungwa hao walitoroka gerezani wakati wakiwa kazini shambani wakiwa
chini ya Ulinzi wa askari wawili sajenti Gaspal na Sanjet Emmanuel na
kwamba hadi kufikia jana(leo jumapili) hakuna hata mfungwa mmoja
aliyekamatwa
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na kamanda wa polisi
mkoani Geita,Leonard Paulo alisema tukio la hivi karibuni la mfungwa anaedaiwa kubaka lilitokea saa 9 alasiri
Februari 26,mwaka huu wakati mwanafunzi huyo akiwa na wenzake wakitoka
kuchanja kuni.
Mfungwa huyo alipowaona wanafunzi hao alijipaka majivu
mwili wote,na wanafunzi hao walipoona hivyo walikimbia na kutawanyika
kila mmoja njia yake na ndipo mmoja wao alianguka chini baada ya
kujikwaa kwenye mti na kisha kumbaka kwa nguvu.
Kwa mujibu kamanda Paulo Mwanafunzi huyo aliumizwa sehemu
za siri,pamoja jicho la kushoto baada ya kupigwa ngumi na mfungo huyo
kwa lengo la kumtaka kutii azima yake ya kumbaka.
Hadi leo hii mfungwa huyo amepandishwa mahakamani na kusomewa mashitaka wawili ambapo shitaka la kwanza ni kubaka na shitaka la pili ni kumjeruhi huyo binti na amekana mashitaka akarudishwa rumande hadi tar 20 march,chini ya hakimu Desdery Kamgisha hakimu mkazi wilaya Geita.
Hadi leo hii mfungwa huyo amepandishwa mahakamani na kusomewa mashitaka wawili ambapo shitaka la kwanza ni kubaka na shitaka la pili ni kumjeruhi huyo binti na amekana mashitaka akarudishwa rumande hadi tar 20 march,chini ya hakimu Desdery Kamgisha hakimu mkazi wilaya Geita.
Na Valence Robert-Geita