WAFANYABIASHARA
wa Manyoni mjini mkoani Singida mume na mke,wametekwa na watu watatu waliojifanya kuwa
ni maafisa usalama wa taifa makao makuu jijini Dar-es-salaam.
Waathirika wa utekaji huo ni Methew Dominik Cheupe (46) na mke wake Selina Methew (42).
Kamanda
wa Jeshi la Polisi mkoani Singida, SACP Geofrey Kamwela amesema tukio
hilo limetokea juzi saa tisa alasiri Manyoni mjini.
Amesema
Faraja George (35) mfanyabiashara wa Dodoma mjini,mganga wa tiba asilia
na mkazi wa mkoa wa Tanga,Saidi Mgolola @Pesa mbili (49) Michael Peter
na Michael Peter (26) mkazi wa Moshi mjini na dereva wa gari
lililotumika katika utekaji huo.
Amesema
siku ya tukio watuhumiwa wakiwa na gari T.242 CBM aina ya toyota
prado,walifika dukani kwa Methew baada ya kudai kuwa wao ni maafisa
usalama taifa,walimwamuru mwenye duka kuwa wanamhitaji Singida mjini kwa
ajili ya mahojiano.
“Methew
aliwaomba maafisa hao bandia kuwa aambatane na mke wake huko kwenye
mahojiano hayo.Baada ya waathirika hao kuingia ndani ya gari,gari hilo
badala ya kuelekea Singida mjini,lilibadili na kuelekea Dodoma”,amesema.
Kamwela
amesema bahati nzuri polisi Manyoni mjini walipata taarifa ya tukio
hilo mapema na wakawasiliana na wenzao wa Bahi mkoani Dodoma ambao
walifanikiwa kuwanasa watuhumiwa hapo kwenye kizuizi.
Amesema
uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo,ni watuhumiwa
kutaka kumwibia mali mfanyabiashara hiyo Methew.Uchunguzi zaidi bado
unaendelea.
Kamwela amesema kuwa mara upelelezi utakapokamilika,watuhumiwa watafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayowakabili.
Na Nathaniel Limu, Singida
Social Plugin