Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Pendo Kona,
amepoteza fahamu na kulazwa katika hospitali ya DDH-Bunda, akidaiwa
kunyweshwa dawa inayosadikika kuwa sumu na waganga wakienyeji ili kuwabaini wezi wang'ombe wake.
Mwanamke huyo mkazi wa Bunda, anadaiwa kunyweshwa dawa hiyo ili awabaini wezi wa ng’ombe wake.
Pendo
inasemekana aliibiwa ng’ombe wawili Januari mwaka huu, na aliamua kwenda
kwa waganga wa kienyeji ili asaidiwe kuwapata wezi wake.
Kamanda wa
Polisi mkoa wa Mara, Fredinand Mtui, alithibitisha kutokea kwa tukio
hilo lilitokea juzi majira ya saa 3:00 asubuhi, katika kijiji cha
Mugeta, wilayani Bunda mkoani Mara.
Kamanda Mtui,
alisema watu hao waliojiita waganga wa kienyenyeji, waliwanywesha
wanafamilia hao watatu, ili wawabaini wezi wa ng’ombe wawili, mali ya
Pendo walioibiwa mwishoni mwa Januari, mwaka huu.
Kamanda Mtui,
alisema mwanamke huyo alipokunywa dawa hiyo, aliishiwa nguvu na kupoteza
fahamu ambapo alipelekwa katika hospitali ya DDH-Bunda kwa matibabu.
Hata hivyo,
alisema Polisi wanamshikilia kijana mmoja ambaye ni mtoto wa mke
mwenzake na Pendo, kwani ndiye anayetuhumiwa kuwaleta waganga hao
waliotoroka baada ya tukio.
Chanzo;Uhuru online
Social Plugin