Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu imesema haina muda wa kujibu porojo zilizotolewa na Askofu wa kanisa la Full Gospel Fellowship, Zachary Kakobe kwani ina kazi kubwa ya kuwatumikia watanzania....
Imesisitiza
kuwa ofisi ya Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu haifanyi kazi za
porojo kama sehemu ya kuendesha utawala wake, badala yake iko
makini kutatua matatizo yanayowakabili wananchi kwa kulinda na
kuheshimu demokrasia na kufuata katiba ya nchi....
Kauli
hiyo inatokana na waraka maalumu unaodaiwa kutolewa na Askofu
Kakobe na kisha kupelekwa Ikulu.Hata hivyo, kurugenzi ya
mawasiliano Ikulu imesema haijathibitisha rasmi kama waraka huo
umefika katika ofisi hiyo.....
Akizungumza
juzi na gazeti la Jambo Leo kwa njia ya simu,Mkurugenzi wa
idara ya mawasiliano Ikulu, Salvatory Rweyemamu alisema serikali
si lazima ijibu Porojo zilizotolewa na Kakobe, kwani Ikulu ni
sehemu nyeti ya kutumikia wananchi katika maswala ya msingi na
yenye tija kwa taifa.....
"Yaani unataka niseme mambo ya porojo badala ya kuelekeza majibu yenye kutatua matatizo ya wananchi",
"Yaani unataka niseme mambo ya porojo badala ya kuelekeza majibu yenye kutatua matatizo ya wananchi",
alisema
na kuongeza kuwa swala hilo lilishajibiwa na kaimu katibu
mkuu ofisi ya waziri mkuu, Dr Florence Turuku ambapo alilitolea
ufafanuzi wa kutosha.
Waraka
huo uliotolewa kwenye vyombo vya habari na Askofu Kakobe
ulikuwa ukieleza namna Ikulu "ilivyotupa kapuni" majina yote ya
wapentekoste waliopendekezwa kuwa wajumbe wa bunge maalumu la
katiba, hivyo kuwafanya wapentekoste takribani milioni 10 kukosa
mwakilishi hata mmoja...
Pia
waraka huo ulidai kuwa baada ya kukosa uwakilishi, Ikulu
ilitoa kauli za kejeli kuwa, haijawahi kupokea jina hata moja
la mpentekoste.
"Ofisi yako imeona kwamba ni haki hata kwa waganga wa kienyeji kuwakilishwa katika bunge hilo kuliko wapentekoste kupata mjumbe hata mmoja", ilisema sehemu ya waraka huo.
"Ofisi yako imeona kwamba ni haki hata kwa waganga wa kienyeji kuwakilishwa katika bunge hilo kuliko wapentekoste kupata mjumbe hata mmoja", ilisema sehemu ya waraka huo.
Hata hivyo baadhi ya wananchi waliohojiwa na gazeti la Jambo Leo walisema Askofu Kakobe amezoea kulumbana na Serikali, hivyo uamuzi wake hauna mashiko.
"Tunajua ana waumini wengi wanaomsikiliza, lakini kwa maswala ya kiserikali ambayo inaaminika haina dini ni vigumu kuitabiria mabaya, kwani yeye kama mchungaji alistahili kukaa pamoja na ofisi husika na si kwenda kunukuu vitabu vitakatifu kwa kuitabiria mabaya serikali", Alisema Patrick Haule ambaye ni Mwinjilisti.
Chanzo: Gazeti la Jambo leo, tarehe 13 march 2014