Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba
jana aliliteka Bunge Maalumu la Katiba mjini Dodoma, alipowasilisha
Rasimu ya Katiba na kushangiliwa katika maeneo mengi nyeti na kupigiwa
kelele katika vipengele vichache vya uraia na ardhi.
Katika hotuba yake ya maneno 14,112 iliyosomwa kwa
saa 3:34, Jaji Warioba aliweka wazi maoni ya wananchi yaliyomo katika
ibara 271 za Rasimu hiyo, ukiwamo muundo wa Muungano wa Serikali Tatu –
Jamhuri ya Muungano, Serikali ya Tanganyika na Serikali ya Zanzibar.
Mwanasheria huyo alijenga hoja zake zilizoisaidia
Tume yake kufikia hitimisho la muundo huo, kwamba ilizingatia maoni ya
wananchi, yakiwamo ya mabaraza ya katiba ya Ofisi ya Makamu wa Rais,
Ofisi ya Waziri Mkuu na Baraza la Wawakilishi Zanzibar ambayo ama moja
kwa moja au kwa tafsiri yalipendekeza muundo wa Serikali Tatu.
Alisema tume hiyo ililazimika kupendekeza muundo
huo kutokana na kero, hoja na malalamiko yaliyotolewa na pande mbili za
Muungano wakati tume hiyo ikukusanya maoni, pamoja na hoja zilizotolewa
miaka ya nyuma na tume mbalimbali.
“Suala la muundo wa Serikali Tatu limechukua
nafasi kubwa katika mjadala tangu tume ilipozindua Rasimu ya Kwanza ya
Katiba. Mjadala wa muundo wa muungano umekuwa mkubwa kiasi cha kufunika
mapendekezo mengine yaliyomo katika Rasimu ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano,” alisema Warioba katika hotuba yake ya aya 191 ambayo
imechapwa kwa ukamilifu ndani ya gazeti hili.
Huku akishangiliwa na baadhi ya wajumbe, Jaji
Warioba alisema kwa tahmini ya tume hiyo, muundo wa Serikali mbili
hauwezi kubaki kwa hali ya sasa.
“Muungano wa Serikali mbili waliotuachia waasisi
siyo uliopo sasa. Umebadilishwa mara nyingi, wakati mwingine bila ya
kufanya mabadiliko kwenye Katiba. Waasisi walituachia Muungano wa nchi
moja yenye Serikali mbili na siyo nchi mbili zenye Serikali mbili,”
alisema.
Alisema muundo wa Serikali mbili unaweza kubaki tu
ikiwa orodha ya mambo ya muungano haitapunguzwa bali itaongezwa na
isipokuwa hivyo Serikali ya Muungano itabaki na rasilimali na mambo ya
Tanzania Bara tu.
“Katika hali hiyo, pande zote mbili zitaendelea
kulalamika. Kwa upande mmoja, Zanzibar itaendelea kulalamika kwamba
Tanzania Bara imevaa koti la Muungano kwa faida yake na kwa upande
mwingine, Tanzania Bara itaendelea kulalamika kwamba mambo yasiyo ya
Muungano ya Tanzania Bara na rasilimali zake, ndizo zimekuwa Muungano,”
alisema.
Warioba alishangiliwa tena na baadhi ya wajumbe
aliposema: “Muundo wa Serikali Tatu haupunguzi uimara wa Muungano na
muungano huo ni wa nchi mbili kwa manufaa ya wananchi, “Faida kubwa
iliyopatikana katika miaka hamsini iliyopita ni kuungana kwa wananchi.”
WALITOA MAONI
WALITOA MAONI
Kuhusu idadi ya waliotoa maoni, alisema watu wengi waliotoa
maoni kuhusu Muungano walijikita katika muundo wake kama njia ya kuondoa
kero,” alisema.
Alifafanua kwamba Tanzania Bara wananchi zaidi ya
39,000 walitoa maoni kuhusu muungano na kati ya hao, 27,000
walizungumzia muundo wake.
Kwa Zanzibar, wananchi karibu wote waliotoa maoni
walijikita kwenye suala la Muungano na kwamba kati ya watu 38,000
waliotoa maoni kuhusu Muungano, 19,000 walitoa maoni kuhusu muundo wake.
“Wananchi waliotoa maoni kuhusu muundo wa Muungano
kwa upande wa Tanzania Bara, asilimia 13 walipendelea Serikali moja,
asilimia 24 Serikali mbili na asilimia 61 waliendekeza Serikali Tatu”
alisema na kuongeza;
Utafiti wa Tume
Alisema kuwa baada ya kuchanganua sababu
mbalimbali zilizotolewa na makundi mbalimbali tume hiyo ilianza kufanya
utafiti wa kina kuhusu muundo wa muungano na matatizo yake tangu
ulipoundwa Aprili 26, 1964, na kutaja tume zilizopendekeza Serikiali
tatu.
Alizitaja tume ya Jaji Francis Nyalali ya mwaka
1993, kundi la Wabunge 55 kutoka Tanzania Bara (G 55) waliopeleka
bungeni hoja ya kuundwa kwa Serikali ya Tanganyika na Tume ya Jaji
Kisanga.
Changamoto Serikali Tatu
Kuhusu Serikali Tatu ambao chama tawala (CCM),
kimekuwa kinaupinga kwa udi na uvumba, Jaji Warioba alisema muundo huo
utakuwa na changamoto zake, ikiwa ni pamoja na kuongezeka kwa gharama
ingawa hazitakuwa kubwa kama inavyofikiriwa.
“Gharama kubwa kwa shughuli za Muungano ni katika
eneo la ulinzi na usalama, yaani jeshi la wananchi, polisi, usalama wa
taifa na mambo ya nje. Gharama hizo hazibadiliki, zinabaki zile zile
bila kujali kama ni muundo wa Serikali mbili au Serikali tatu,” alisema.
Alisema tangu Muungano uundwe, Serikali ya
Muungano na Serikali ya Zanzibar zimekuwa zikiongeza wizara, mikoa,
wilaya na taasisi mbalimbali za kiutawala ili kuleta ufanisi na hivyo
kuongeza matumizi ya Serikali.
“Tume imependekeza kodi ya bidhaa iwe ya Muungano,
pia mapato yasiyo ya kodi, mikopo na michango ya nchi washirika. Ushuru
wa bidhaa utakidhi sehemu kubwa ya gharama za muungano,” alisema na
kuongeza:
Via>>mwananchi
Via>>mwananchi
Social Plugin