Nb-picha haiendani na habari |
Mahakama ya
Wilaya ya Mpanda Mkoa wa Katavi imemuhukumu
Wiliamu George 32 Mkazi wa Mtaa
wa Nsemlwa Wilaya ya Mpanda kifungo cha miaka 30
jela baada ya kupatikana na hatia ya kumlawiti kijana mwenzie 22 Mkazi wa Mtaa wa Mpandahoteli baada ya
kumnywesha pombe ya kienyeji kupita kiasi.
Hukumu hiyo
ilitolewa hapo jana
na Hakimu mkazi
mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya
Mpanda Chiganga Ntengwa na hukumu
hiyo kuvuta hisia za watu
mbalimbali wa maeneo ya mji wa Mpanda na Mkoa wa Katavi.
Hukumu hiyo ilitolewa na Hakimu wa mahakama
hiyo baada ya mahakama
kuridhika na ushahidi
uliotolewa mahakamani hapo
wa upande wa mashitaka na upande wa
utetezi.
Katika kesi hiyo hapo
awali mwendesha mashitaka mkaguzi wa jeshi la polisi Ally Mbwijo alidai mahakamani hapo kuwa mshitakiwa
alitenda kosa hilo hapo Novemba
21 mwaka jana majira ya kumi na
mbili jioni katika mtaa wa Mpanda Hotel.
Mshitakiwa siku
hiyo ya tukio kabla ya kutenda
kosa hilo la kumlawiti
kijana huyo alidaiwa kunywesha pombe ya kienyeji aina ya komoni ,
walikuwa wakichanganya na bia nyumbani kwa mwanamke aliyekuwa akiwauzia
pombe aliyetambulika kwa
jina moja la Lita katika mtaa huo wa Mpanda hotel.
Ilielezwa na
mwendesha mashitaka Ally Mbwijo alisema kuwa mshitakiwa
baada ya kuona mwenzake
anatoka anatoka nje kwenda
kujisaidia alimwagiza dukani Lita
aende akamnulie sigara.
Alieleza mahakama
baada ya kijana huyo amba ejina lake limehifadhiwa kurudi
ndani aliendelea na kunywa pombe
ambayo alikuwa ameishaiweka kwenye chupa yake na
ndipo alipoteza fahamu na mshitakiwa alitumia nafasi huyo
kumwingilia kinyume cha maumbile
yake huku akiwa amemlaza kwenye kochi.
Mwendesha mashitaka
alieleza Lita alipotoka
dukani alimkuta mshitakiwa akiwa amekaa karibu na kijana
huyo ambae alikuwa amevuliwa nguo yake ya saruali
na akiwa hajitambui na sehemu zake za
matakoni zikiwa na mbegu
za kiume.
Mshitakiwa baada ya kufanya kitendo hicho siku iliyofuata alimtuma
mama yake mzazi aende kwa kijana
huyo akamwombee samahani kwa kile alichoeleza
kuwa anahofia kufungwa jela.
Baada ya mama
mshitakiwa Wiliamu George
kumwombea msamaha kwa kijana aliyelawitiwa
alikubali kumsamehe mshitakiwa
kwa kuhofia kupata aibu.
Mshitakiwa baada
ya kusamehewa alianza kumtangaza kijana huyo
kwa rafiki zake na kuwafahamisha kuwa kijana huyo ni shemeji yao
kitendo ambacho kilimkasirisha kijana
huyo na kuamua kwenda kituo cha polisi kutoa taarifa ya kulawitiwa kwake na Mshitakiwa Wiliamu George.
Hakimu mkazi
mfawidhi Chiganga Ntengwa kabla ya kutoa hukumu hiyo aliiambia mahakama kuwa mahakama imemtia hatiani mshitakiwa Wiliamu
George kwa kosa la kumwingilia
kijana huyo kinyume na maumbile
yake hivyo mahakama inatoa nafasi kwa mshitakiwa kama anasababu ya msingi ya
kuishawishi mahakama impunguzie adhabu aieleza mahakama hiyo.
Katika utetezi
wake mshitakiwa aliiomba mahakama imwachie huru kwani yeye hakutenda kosa hilo na pia umri wake
bado ni kijana mdogo na wazazi wake bado wanamtegemea maombi ambayo yalipingwa vikari na mwendesha
mashitaka.
Hakimu Chiganga
baada ya kusikiliza utetezi huo aliiambia mahakama kuwa mshitakiwa amehukumiwa na mahakama
baada ya kupatikana na hatia ya kumwingilia kinyume na maumbile
kijana huyo na anahukumiwa na adhabu ya
kifungu cha sheria namba 235 sura ya 20 ya mwaka 2009 hivyo Wiliamu
George mahakama imehukumu kutumikia jela kuanzia jana kifungo cha miaka 30 jela.
Na Walter Mguluchuma-Mpanda Katavi