Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KIJANA ACHOMWA MOTO HUKO KAHAMA KWA KUHISIWA KUWA NI MWIZI,ALIKUWA NA MAPANGA MAWILI KWENYE KOTI KUBWAAAA

Kijana mmoja anayesadikiwa kuwa ni mwizi ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja amefariki dunia baada ya kuchomwa moto na Wananchi wanaodaiwa kuwa na hasira, katika kijiji cha Kagongwa Wilayani Kahama Mkoani Shinyanga.

Kwa mujibu wa mashuhuda tukio hilo limetokea jana majira ya saa mbili usiku kufuatia marehemu kujaribu kukodisha Usafiri wa pikipiki maarufu kama bodaboda kwa lengo la kwenda Kijiji jirani cha Mwankumba. 

Imeelezwa kuwa madereva hao wa bodaboda walishtuka kuoa mtu huyo akiwa amevaa koti kubwa, ndipo walipomuliza ili kujua vitu alivyobeba, na ndipo alipojaribu kukimbia kabla ya kukamatwa na wananchi waliokuwepo katika eneo hilo.

Hata hivyo baada ya Kijana huyo kukamatwa amekutwa akiwa na Mapanga mawili aliyoyaficha ndani ya koti, jambo lililopelekea wananchi hao kuchukua jukumu la kumchoma moto wakimuhisi kujihusisha na matukio ya wizi.

Baada ya tukio hilo Jeshi la Wilayani Kahama limefika eneo hilo na kuchukua mwili wa marehemu ambao kwa sasa umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama, huku uchunguzi zaidi wa tukio hilo ukiendelea.
credit-eddy blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com