TGNP MTANDAO WAANZA KUTOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA
Thursday, March 27, 2014
TGNP Matandao leo umeanza kutoa
mafunzo kwa waandishi wa habari takribani 20 kuwajengea uwezo wa
kuandika mambo mbalimbali kama vile masuala ya jinsia,rasimu ya pili ya
katiba ,mafunzo hayo yatakayodumu kwa muda wa siku tatu yanafanyika
katika Ukumbi wa Papa Paulo wa 2,katika kanisa katoliki la Ngokolo mjini
Shinyanga.Anayezungumza ni kaimu meneja wa habari na mawasiliano
kutoka TGNP Mtandao bi Kenny Ngomuo ambaye alitaja
na kuelezea mapungufu ambayo TGNP Mtandao imeyaona katika rasimu ya pili ya
katiba. Alisema miongoni mwa mapungufu hayo ni kuhusu lengo hasa la
katiba lakini pia akazungumzia kuhusu haki za wanawake kwani rasimu
ya pili ya katiba haijabainisha zaidi kuhusu haki za wanawake.Bi Ngomuo
alisema TGNP Mtandao inapendekeza haki za wanawake zipanuliwe yaani haki zao
ziongezwe,kuwepo na haki ya uzazi salama,haki ya likizo wanapokuwa
wajawazito n.k.
Washiriki
katika warsha hiyo wakifanya kazi za kikundi kama walivyoelekezwa na
maafisa hao kutoka TGNP Mtandao,kulia ni Bi Moshi Ndugulile kutoka Radio
Faraja kulia ni bwana Kadama Malunde wa gazeti la Zanzibar leo na
mtandao wa malunde1 blog
Bi Veronica Natalis kutoka Radio Faraja akiwasilisha kazi ya kundi lake wakati wa warsha ya TGNP Mtandao ambapo pamoja na mambo mengine maafisa hao kutoka TGNP Mtandao waliwataka waandishi wa habari kuandika habari zao kwa kuzingatia usawa wa jinsia
Kushoto ni bi Anna Sangai ambaye ni afisa kutoka TGNP Mtandao anayehusika na masuala ya utafiti,ushawishi na ujenzi wa nguvu za pamoja akigawa tisheti kwa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo,tisheti hizo zimeandaliwa na TGNP Mtandao na huyo kulia anayepokea tisheti ni bwana Chibura Makorongo mwandishi wa habari gazeti la Uhuru na Mzalendo.Bi Sangai alisema matatizo ya kijinsia yanatokana na sababu nyingi
kama vile umaskini,mila na desturi,masharti ya wahisani na kwamba vita
dhidi ya ukatili wa kijinsia itaisha endapo kutakuwa na sera pamoja na
mikakati mizuri dhidi ya matatizo hayo hasa hasa kuwa na katiba nzuri
inayogusa maisha ya kila mtu.
Katika warsha hiyo ya siku tatu waandishi wa habari watakuwa na muda mzuri wa kutafakari nini wajibu wao katika kuripoti masuala kadha wa kadha hususani matatizo ya kijinsia ambayo ni kikwazo cha maendeleo kwa wanawake kama vile kubakwa,kubebeshwa ujauzito wangali wadogo ama wakiwa shule,huduma mbovu katika hospitali,vituo vya afya n.k.Lakini pia kutafakari namna ya kuandika habari zinazohusu makundi maalum kama vile wazee,watoto,walemavu .k
Bwana Faustine Kasala kutoka Radio Faraja ya Shinyanga akisikiliza kwa umakini kuhusu mapendekezo ya TGNP Mtandao katika katiba ijayo,ambapo pamoja na mambo mengine TGNP inataka kuwepo na haki za wanawake wenye ulemavu kwani wamesahaulika katika rasimu ya pili ya katiba,na kutokana na wanawake hao kukabiliwa na changamoto nyingi wao wanapendekeza wanawake wenye ulemavu wawe na haki ya kutobaguliwa,haki ya kufikia huduma mbalimbali za kijamii,kupatiwa huduma za uzazi salama kulingana na hali yao,haki ya kulindwa n.k.
Washiriki
wa semina hiyo wakijadiliana katika makundi yao kulingana na kazi
walizokuwa wamepewa kujadili kuhusu masuala ya kijinsia
Bwana Masanja Thomas kutoka Radio Sibuka Fm akiwasilisha kazi ya kundi lake kuhusu mapungufu wanayoyaona katika rasimu ya pili ya katiba hapa nchini,Thomas alisema rasimu ya pili ya katiba haijabainisha wazi kuhusu haki za wanawake wazee ambao mfano katika mkoa wa Shinyanga wanakumbana na changamoto ya kuuawa kwa ksingizio cha kuwa ni wachawi lakini pia akazungumzia kuhusu tafsiri ya mtoto kwani rasimu ya pili ya katiba haijabainisha na hivyo kupendekeza katiba ya nchi itaje kuwa mtoto ni mtu yeyote aliye chini ya miaka 18
Kulia ni Steve Kanyefu maarufu kwa jina la BWANA MICHAPO akiwa na Veronica Natalis wote kutoka Radio Faraja wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika semina hiyo
Semina inaendelea
Bwana Shaaban Alley wa Star/Radio Free Africa ambaye pia ni mkurugenzi wa shalleyhabari.blogspot.com akichukua mawili matatu katika semina hiyo ya siku tatu kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin