Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TGNP MTANDAO WAANZA KUTOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA

TGNP Matandao leo umeanza kutoa mafunzo kwa waandishi wa habari takribani 20 kuwajengea uwezo wa kuandika mambo mbalimbali kama vile masuala ya jinsia,rasimu ya pili ya katiba ,mafunzo hayo  yatakayodumu kwa muda wa siku tatu yanafanyika katika Ukumbi wa Papa Paulo wa 2,katika kanisa katoliki la Ngokolo mjini Shinyanga.Anayezungumza ni kaimu meneja wa habari na mawasiliano kutoka TGNP Mtandao bi Kenny Ngomuo ambaye alitaja na kuelezea mapungufu ambayo TGNP Mtandao imeyaona katika rasimu ya pili ya katiba.
Alisema miongoni mwa mapungufu hayo ni kuhusu lengo hasa la katiba lakini pia akazungumzia  kuhusu haki za wanawake kwani rasimu ya pili ya katiba haijabainisha zaidi kuhusu haki za wanawake.Bi Ngomuo alisema TGNP Mtandao inapendekeza haki za wanawake zipanuliwe yaani haki zao ziongezwe,kuwepo na haki ya uzazi salama,haki ya likizo wanapokuwa wajawazito n.k.
Washiriki katika warsha hiyo wakifanya kazi za kikundi kama walivyoelekezwa na maafisa hao kutoka TGNP Mtandao,kulia ni Bi Moshi Ndugulile kutoka Radio Faraja kulia ni bwana Kadama Malunde wa gazeti la Zanzibar leo na mtandao wa malunde1 blog
Bi Veronica Natalis kutoka Radio Faraja akiwasilisha kazi ya kundi lake wakati wa warsha ya TGNP Mtandao ambapo pamoja na mambo mengine maafisa hao kutoka TGNP  Mtandao waliwataka waandishi wa habari kuandika habari zao kwa kuzingatia usawa wa jinsia

Kushoto ni bi Anna Sangai ambaye ni afisa kutoka TGNP Mtandao anayehusika na masuala ya utafiti,ushawishi na ujenzi wa nguvu za pamoja akigawa tisheti kwa waandishi wa habari waliohudhuria mafunzo hayo,tisheti hizo zimeandaliwa na TGNP Mtandao na huyo kulia anayepokea tisheti ni bwana Chibura Makorongo mwandishi wa habari gazeti la Uhuru na Mzalendo.Bi Sangai alisema matatizo ya kijinsia yanatokana na sababu nyingi kama vile umaskini,mila na desturi,masharti ya wahisani na kwamba vita dhidi ya ukatili wa kijinsia itaisha endapo kutakuwa na sera pamoja na mikakati mizuri dhidi ya matatizo hayo hasa hasa kuwa na katiba nzuri inayogusa maisha ya kila mtu.
Katika warsha hiyo  ya siku tatu waandishi wa habari watakuwa na muda mzuri wa kutafakari nini wajibu wao katika kuripoti masuala kadha wa kadha hususani  matatizo ya kijinsia ambayo ni kikwazo cha maendeleo kwa wanawake kama vile kubakwa,kubebeshwa ujauzito wangali wadogo ama wakiwa shule,huduma mbovu katika hospitali,vituo vya afya n.k.Lakini pia kutafakari namna ya kuandika habari zinazohusu makundi maalum kama vile wazee,watoto,walemavu .k
Bwana Faustine Kasala kutoka Radio Faraja ya Shinyanga akisikiliza kwa umakini kuhusu mapendekezo ya TGNP Mtandao katika katiba ijayo,ambapo pamoja na mambo mengine TGNP inataka kuwepo na haki za wanawake wenye ulemavu kwani wamesahaulika katika rasimu ya pili ya katiba,na kutokana na  wanawake hao kukabiliwa na changamoto nyingi wao wanapendekeza wanawake wenye ulemavu wawe na haki ya kutobaguliwa,haki ya kufikia huduma mbalimbali za kijamii,kupatiwa huduma za uzazi salama kulingana na hali yao,haki ya kulindwa n.k.
Washiriki wa semina hiyo wakijadiliana katika makundi yao kulingana na kazi walizokuwa wamepewa kujadili kuhusu masuala ya kijinsia

Bwana Masanja Thomas kutoka Radio Sibuka Fm akiwasilisha kazi ya kundi lake kuhusu mapungufu wanayoyaona katika rasimu ya pili ya katiba hapa nchini,Thomas alisema rasimu ya pili ya katiba haijabainisha wazi kuhusu haki za wanawake wazee ambao mfano katika mkoa wa Shinyanga wanakumbana na changamoto ya kuuawa kwa ksingizio cha kuwa ni wachawi lakini pia akazungumzia kuhusu tafsiri ya mtoto kwani  rasimu ya pili ya katiba haijabainisha na hivyo kupendekeza katiba ya nchi itaje kuwa mtoto ni mtu yeyote aliye chini ya miaka 18
Kulia ni Steve Kanyefu maarufu kwa jina la BWANA MICHAPO akiwa na Veronica Natalis wote kutoka Radio Faraja wakifuatilia kilichokuwa kinajiri katika semina hiyo

Semina inaendelea
Bwana Shaaban Alley wa Star/Radio Free Africa ambaye pia ni mkurugenzi wa shalleyhabari.blogspot.com akichukua mawili matatu katika semina hiyo ya siku tatu kwa waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com