Kilichojiri Shinyanga Leo!!! NEEMA YAANGUKA KATIKA KIJIJI CHA MWAMALILI NA SESEKO VILIVYOPO KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA,WIKI YA MAJI DUNIANI YALETA FARAJA TATIZO LA MAJI
Monday, March 17, 2014
mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga (wa nne kutoka kulia)baada ya kukata utepe kama ishara ya kuzindua rasmi mradi wa maji katika kijiji cha Mwamalili na Seseko katika kata ya Mwamalili katika manispaa ya Shinyanga leo huku viongozi mbalimbali wakishuhudia tukio hilo ikiwa ni katika kuadhimisha wiki ya maji duniani.
Ujenzi wa Mradi wa maji katika kijiji cha Mwamalili na Seseko
umetekelezwa na mkandarasi mzawa kutoka kampuni ya PNR SERVICES CO LTD
ya Dar es salaam ambapo utekezaji rasmi wa mradi umeanza mwaka jana na
umekamilika asilimia 98 na utakamilika tarehe 31 mwezi huu.Kazi
zilizotekelezwa ni ujenzi wa vituo 21 vya kuchotea maji,uchimbaji mitaro
na ulazaji wa mabomba urefu wa mita 27,054,ujenzi wa chemba kwa ajili
ya valve za kutolea hewa na kusafishia mabomba samabamba na ujenzi wa
matanki matatu ya mfano kwa ajili ya uvunaji wa maji ya mvua yenye ujazo
wa mita za ujazo 5,3 na 1.Matanki hayo yamejengwa kwenye tasisiza
serikali kama vile shule na zahanati zilizopo kwenye vijiji husika
Ni katika kijiji cha Mwamalili kata ya Mwamalili katika manispaa ya Shinyanga ambako leo mkuu wa mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Ally Nassoro Rufunga amezindua mradi wa maji ya ziwa Victoria katika kijiji cha Mwamalili na Seseko katika kuadhimisha wiki ya maji duniani kote ambayo hufanyika kuanzia tarehe 16 mwezi Machi hadi Machi 22 ambayo ndiyo siku ya maji duniani na katika mkoa wa Shinyanga kilele chake kitafanyika katika eneo la Kagongwa wilayani Kahama yakiongozwa na kauli mbiu UHAKIKA WA MAJI NA NISHATI,lakini mkoa wa Shinyanga hivi sasa una kauli mbiu yake isemayo UCHUMI IMARA SHINYANGA,SHINYANGA UCHUMI IMARA.Pichani aliyeshika bomba la maji ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga mara baada ya kuweka jiwe la msingi katika mradi huo wa maji.
Wa
kwanza kulia ni diwani wa viti maalum kata ya Mwamalili bi Grace
Mihambo,akifuatiwa na diwani wa kata hiyo Paul Machela wakisaidiana na
mkuu wa mkoa wa Shinyanga mheshimiwa Rufunga wakimtwisha ndoo ya maji ya
mradi uliozinduliwa na mkuu huyo wa mkoa ikiwa ni katika kuadhimisha
wiki ya maji duniani.Ujenzi wa mradi huo wa maji vijiji vya Mwamalili na
Seseko gharama yake kuu ni shilingi 538,178,200/= mradi ambao
utahudumia watu wapatao 5334 kwa vijiji vya Mwamalili watu 3262 na
Seseko watu 2072 na kila kaya inachangia shilingi elfu 35.
Katikati ni diwani wa kata ya Mwamalili Paul machela akizungumza mara baada ya uzinduzi wa mradi huo wa maji,ambapo aliipongeza serikali kwa kusikia kilio cha wakazi wa eneo hilo kuwa na tatizo la maji kwa muda mrefu na sasa huduma ya maji imesogezwa ambapo hapo awali walikuwa wanafuata huduma ya maji mbali mfano eneo la Old Shinyanga na maeneo mengine .Katika kufanikisha mradi huo bado kuna kasi ndogo ya wananchi kuchangia fedha za uendeshaji wa mradi kwani hadi sasa wananchi wameweza kuchangia shilingi 320,000/= kati ya shilingi 13,454,455/= ambayo ni asilimia 2.5 ya gharama ya mradi zinazotakiwa kutolewa na wananchi
kuchangia mradi huo wa maji huku akiwataka kutunza mradi huo na kwa wale ambao hadi sasa hawatoa michango yao akaliagiza jeshi la sungusungu katika kijiji cha Mwamalili kufuatilia michango yao pesa ambazo zitasaidia kuendesha mradi huo wa maji ya ziwa victoria ambayo yatasambzwa na mamlaka ya maji safi na taka katika manispaa ya Shinyanga -SHUWASA.Mkuu huyo wa mkoa akatumia fursa hiyo kuwaelimisha wananchi kuhusu umhimu wa kuchangia miradi ya maendeleo huku akiwataka wananchi kuondoa dhana ya kwamba mkoa wa Shinyanga ni maskini bali kinachosumbua ni tatizo la fikra na maamuzi akitolea mfano wa kutumia kuku wanaowafuga ili kuchangia miradi ya maji
Maafisa mbalimbali wa ulinzi na usalama wakifuatilia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga
Aliyesimama ni mwenyekiti wa kamati ya maji katika kijiji cha Mwamalili Elisha Mahalala akijibu swali la mkuu wa mkoa aliyetaka kujua kwanini kasi ya uchangiaji kwa wananchi ndogo katika kijiji hicho ambapo hadi sasa wananchi wamechanga shililngi 320,000/= kati ya shilingi 13,434,455/= zinazohitajika kutoka kwa wananchi.Mwenyekiti huyo wa kamati kasi ndogo ya uchangiaji inatokana na tatizo la njaa katika vijiji hivyo ingawa alisema tayari wamekubalina kukamilisha michango yao hadi kufikia mwishoni mwa mwezi huu.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin