Mtu
mmoja amekufa papo hapo na wengine 22 kujeruhiwa vibaya baada ya basi
la kampuni ya saibaba walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Dar es
salaam kwenda Kyela mkoani Mbeya kupinduka katika kijiji cha Mwambegele
wilayani Rungwe.
Safari
ya basi la kampuni ya Saibaba lenye namba za usajili T 973 AVW kutoka
jijini Dar es Salaam kwenda wilayani Kyela imeishia kwenye kona kali ya
Mwambegele wilayani Rungwe, baada ya basi hilo kupinduka, ambapo mkuu
wa wilaya Rungwe Crispine Meela ni miongoni mwa watu ambao wamewahi
kufika kwenye eneo la tukio na hapa anaelezea chanzo cha ajali hiyo.
Mganga mkuu wa hospitali ya wilaya ya Rungwe waliokolazwa majeruhi,Mandana Stanford
Mwakatage amethibitisha kupokea mwili wa mtu mmoja na majeruhi 22 wa
ajali hiyo huku akisema kuwa baadhi ya majeruhi hali zao bado sio za
kuridhisha.
Imeelezwa kuwa mwendo kasi wa basi hilo ndio
umewasababishia ajali ambayo imesababisha kifo cha dereva wa basi hilo.