WATU wanne wameuawa mkoani Mwanza kwa tuhuma za wizi wa ng’ombe Katika eneo la Igwambiti kata ya Buhongwa Wilaya ya Nyamagana.
Akizungumza
na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza Valentino
Mlowola amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jana majira ya saa
11 alfajiri ambapo wananchi walipata taarifa ya kuwepo kwa wizi wa
ng’ombe katika kitongoji cha Mtende.
Aidha,
kamanda Mlowola amewataja waliofariki kuwa ni pamoja na Ezekiel Lucas
(27), Kusekwa Lucas (25), Masumbuko Kisinza (30) na Mafisi Mwita (26)
ambao walishambuliwa na wananchi kwa silaha za jadi kinyume cha sheria.
Hata hivyo, amesema tayari Jeshi la Polisi linawashikilia watu watatu kwa kukutwa na silaha mbalimbali ambazo zimesadikiwa kutumika katika tukio hilo ,huku uchunguzi wa tukio hilo ukiendelea.
Social Plugin