Watake, wasitake kuanzia sasa kila mwanamume atalazimika kunyoa nywele zake kwa mtindo anaoupenda Rais Kim Jong- un.
Kiongozi huyo kijana, aliyerithi
wadhifa huo baada ya kifo cha baba yake, hana mzaha hasa kutokana na nia
yake ya kujenga mfumo mpya wa utawala ambao matakwa yake tu ndiyo ya
kufuatwa.
Ni wiki mbili sasa tangu serikali ya
nchi hiyo kutoa agizo linalowataka wanaume kunyoa kama rais wao, huku
wanawake nao wakielekezwa kutengeneza nywele zao kwa aina 18 tofauti na
si zaidi ya hapo.
Hilo ni moja ya maagizo yenye utata
kuwahi kutolewa chini ya utawala wake, ambapo amekuwa akifanya jitihada
za kujijengea mizizi, ikiwamo kuwaondoa na kuwaadhibu wale waliokuwa
katika utawala wa baba yake wanaoonekana kutokubaliana na aina yake ya
uongozi.
Mapokezi tofauti
Hata hivyo, japokuwa staili yake ya
unyoaji wa nywele imekuwa sehemu ya utambulisho wake na inafahamika na
kila mmoja, agizo hilo limekuwa na mapokeo tofauti.
“Namna ya unyoaji wake wa nywele
inavutia, kwa wanaoipenda. Lakini haiwezi kumpendeza kila mmoja
atakayeiiga kwa kuwa maumbo ya vichwa yako tofauti kutokana na
maumbile,” alieleza raia mmoja akinukuliwa na Radio Free Asia ya Korea
Kusini.
Raia mwingine wa Korea Kaskazini
ambaye anaishi nchini China, alieleza kwamba aina hiyo ya unyoaji nywele
kwa raia waliopo China inaweza kuonekana kama uhuni.
“Hadi katikati ya miaka ya 2000
tulikuwa tukiitaja aina hiyo ya unyoaji wa nywele kama ‘mtindo wa wahuni
wa China,” alisema raia huyu alipohojiwa na gazeti la Korea Times.
Hadi sasa, wanaume wa Korea Kaskazini wana aina 10 za unyoaji zilizowahi kuamriwa na Serikali yao.
Wanaume wamekuwa wakitakiwa kuwa na
nywele fupi za wastani zenye urefu wa inchi mbili na wametakiwa pia
kuzipunguza kila baada ya siku 15.
Via>>Babamzazi.com
Social Plugin