Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Majonzi makubwaa!! WATOTO WATEKETEA KWA MOTO WAKIWA WAMELALA -TABORA MJINI


Watoto hao walipokuwa wamelala na kuteketea kwa moto ambao chanzo chake inadhaniwa kuwa ni hitilafu za umeme.
Miili ya watoto wawili wa familia moja Daniel Paul(8)na mdogo wake Emmanuel Paul(3) ambao wamepoteza maisha baada ya nyumba waliokuwa wakiishi kuteketea kwa moto huku wakiwa wamelala ndani majira ya saa moja asubuhi peke yao  huko eneo la mtaa wa Rufita Mwanza road Tabora mjini.
Kamanda wa Polisi wilaya ya Tabora  OCD  Samwel Mwampashe akizungumza na wananchi wakati wa tukio hilo la kusikitisha lililotokea na kupoteza maisha ya watoto hao.
Katikati alijishika kichwani ni Paul Daniel ambaye baba wa watoto hao walipoteza maisha akiangalia maiti za watoto wake hao wawili muda mfupi mara baada ya kufika eneo la tukio ambapo maswali mengi yalizuka baba huyo alikuwa wapi wakati watoto wanateketea kwa moto ndani ya nyumba.
Mkuu wa wilaya ya Tabora Bw.Suleiman Kumchaya alifika eneo la tukio mapema wakati Kikosi cha Zimamoto kikimalizia uzimaji wa moto na kuwatoa watoto hao ambao tayari walikuwa wamekwisha kufa.

Huyu mama na mtoto walisalimika  katika tukio hilo la moto ambao walikuwa kwenye vyumba vingine
Baadhi ya Samani ziliteketea vibaya kwa moto huo.PICHA ZOTE KWA HISANI YA KAPIPIJ BLOG

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com