Kijana mmoja mkazi wa Kijiji cha Mabalanga wilayani Kilindi,mkoani Tanga
Hassani Said (28) amemuua kwa kumkata na jembe kichwani bibi yake,
lakini baadaye akauawa na wananchi wa eneo hilo.
Mkazi mmoja wa kijiji
hicho Omari Waziri alisema kuwa Februari 25 mwaka huu kijana huyo
alikuwa akitoka shamba na bibi yake aliyefahamika kwa jina la Mwajuma
Waziri (62), lakini ghafla alinyanyua jembe alilobeba na kumkata
kichwani bibi yake na kufariki dunia.
Alisema kuwa baada ya kufanya mauaji hayo, Hassan
alijificha kwenye nyumba iliyo jirani na wananchi walipopata taarifa
akiwemo babu yake, Mkomwa Mkombozi (72) walikwenda kwa lengo la
kumkamata.
Katika jitihada za kumkamata, mtuhumiwa alitoa
panga na kumjeruhi vibaya Mkombozi ambaye anaendelea kupata matibabu
kwenye Hospitali ya Handeni.
Baada ya kumtia mikononi, wananchi walimshambulia kwa zana mbalimbali hadi kumuua.
Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zilidai kuwa, mtuhumiwa alikuwa na matatizo ya akili.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Costantine
Massawe alipotafutwa na kuhusu tukio hilo, alisema hafahamu lolote kwa
vile yuko nje ya ofisi.
Chanzo-Mwananchi
Chanzo-Mwananchi
Social Plugin