Mfano wa Kuigwa !! KAMPUNI YA EASY FLEX PRODUCTION YA MJIN SHINYANGA YAANDAA HAFLA KUSAIDIA KAMBI YA WAZEE KOLANDOTO NA KITUO CHA WATOTO WENYE ULEMAVU CHA BUHANGIJA KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA
Monday, March 24, 2014
Kulia ni bi Happiness Mwaja Kihama (Mkurugenzi wa Easy Flex production )ambaye ni
mratibu
wa mradi wa kuwasaidia wazee kuchangia
kambi ya Kolandoto na Buhangija kutoka
kampuni ya Easy FlexProduction
ya mjini
Shinyanga inayojihusisha na shughuli za uzalishaji wa kazi za wasanii
katika mfumo wa Sauti na Video wakati akizungumza wakati wa mkutano wao
na waandishi wa habari
leo mjini Shinyanga katika ukumbi wa Karena Hotel,ambapo amesema kampuni
yake kwa kushirikiana na uongozi wa mkoa pamoja na wadau mbalimbali
wameandaa hafla ya chakula cha wahisani.Amesema hafla hiyo inalengo la
kuiamsha jamii na kukusanya fedha pamoja na mali kwa lengo la kuwasaidia
jamii ya wazee waishio kwenye kambi ya Kolandoto pamoja na watoto wa
shule ya maalum ya walemavu wa ngozi,wasioona,wasiosikia ya Buhangija
mjini Shinyanga,ambapo halfa hiyo itafanyika tarehe 29 mwezi huu, katika
ukumbi wa Karena hoteli kuanzia saa nane mchana,ambapo mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Nassoro Rufunga.
Wa kwanza kulia ni
mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya hafla hiyo Sospeter Wilson
Ntoke ambaye ameitaka jamii kujitokeza kusaidia watu wasiojiweza na kuacha dhana potofu ya kutegemea
watu kutoka nje ya nchi kwamba wao ndiyo
wanapaswa kutoa misaada.Hivi karibuni kampuni ya Easy Flex production ilitembelea
kambi
ya wazee ya Kolandoto pamoja na kituo cha walemavu wa ngozi Albino kilichopo Buhangija
mjini Shinyanga na kujionea changamoto mbalimbali zilizopo katika vituo hivyo
na kukumbana na changamoto ya wazee( wanamme na wanawake) kutumia choo kimoja
katika kambi ya wazee ya Kolandoto.
Mbali na changamoto ya choo ,kambi wazee ya Kolandoto inakabiliwa na ukosefu wa
jiko,vyandarua, pamoja na vitanda ambapo wazee hao wanalalia vitanda vibovu
vilivyochoka vyamiaka ya 70 ambavyo si salama kwa afya zao.
Waandishi wa habari wakichukua mawili matatu kwenye mkutano huo.Pia
baada
ya kampuni ya Easy Flex Production kutembelea kituo cha kulea watoto wenye
ulemavu wa ngozi cha Buhangija jumuishi chenye watoto zaidi ya 250 walijionea halihalisi ya kituo hicho kinachokabiliwa na changamoto
ya ukosefu wa chakula, uhaba wa mabweni mavazi, vifaa vya kufanyia usafi,vitanda
ambapo kitanda kimoja cha futi 2 kinalaliwa na watoto wawili.
Waandishi wa habari wakiwa katika ukumbi wa mikutano katika hoteli ya Karena leo mjini Shinyanga
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin